MDAU WA ELIMU EMILIAN MSIGWA AMESEMA KIMSINGI SHULE HIYO NI YA VIPAJI MAALUMU INACHUKUA WANAFUNZI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI LAKINI ANASHANGAZWA KUONA UTARATIBU WA HALMASHAURI KUWACHANGISHA MICHANGO WANANCHI WA ENEO HUSIKA HUKU WAO WATOTO HAWASOMESHI KWENYE SHULE HIYO
HUYU NI MIONGONI MWA WALIONYANYASIKE KWA KUPIGWA BAADA YA KUSHINDWA KUCHANGIA MCHANGO WA SHULE HIYO
Wananchi Wa Vijiji Vya Kata Ya Ihanga Wameilalamikia Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kwa
Kuwatoza Michango Ya Ujenzi Wa Majengo Ya Shule Ya Sekondari Ya Wasichana Anne
Makinda Ikiwa Watoto Wa Kutoka Kata Hiyo Hawasomi Katika Shule Hiyo Ambapo
Wamesema Wamekosa Imani Na Shule Hiyo Kwamba Huenda Wanachangia Shule Ya Mtu
Binafsi.
Wakizungumza Na Mtandao Huu Wananchi Hao Wamesema Changamoto Inayowakabili Ni
Kulazimishwa Kuchangia Michango Ya Shilingi Elfu 32 Kwaajili Ya Ujenzi Wa Vyoo ,
Madarasa Na Miundombinu Mingine Ya Shule Huku Wanaoshindwa Kutoa Michango Hiyo
Wanadhalilishwa Kwa Kupelekwa Rokapu Na Kupewa Adhabu Ikiwa Hawanufaiki Na Shule
Hiyo.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Wamekosa Imani Na Uwepo Wa Shule Ya Sekondari Ya
Wasichana Ya Anne Makinda Kuitwa Ya Kata Na Wananchi Wa Kata Hiyo Kushiliki
Uchangiaji Wa Michango Mbalimbali Huku Watoto Wao Wakipelekwa Kusoma Shule Ya
Sekondari Ya Kata Ya Kifanya Licha Ya Kata Yao Kuwa Na Shule Ya Sekondari Ya Kata.
Wamesema Kuwa Wanafunzi Wanaosoma Katika Shule Ya Sekondari Ya Wasichana Ya Anne
Makinda Wanatoka Sehemu Za Mbali Ambapo Watoto Wa Kata Ya Ihanga Wanaosoma Shule
Hiyo Hata 10 Hawafiki Huku Ada Ikidaiwa Kutoza Zaidi Ya Shilingi Laki Nane Kwa Kila
Mwanafunzi Jambo Linasababisha Wananchi Hao Kukosa Imani Na Shule Hiyo .
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kwa Niaba Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji
Wa Njombe Ilumineta Mwenda,Afisa Elimu Shule Za Sekondari Venance Msungu
Amekanusha Madai Yanayotolewa Na Wananchi Hao Nakwamba Shule Ya Wasichana Ya
Anne Makinda Inachukua Wanafunzi Wa Kutoka Kata Mbalimbali Za Halmashauri Ya Mji Na
Kipaumbele Ni Kata Ya Ihanga.
Msungu Amesema Shule Ya Sekondari Ya Anne Makinda Inafadhiliwa Na Mashirika
Mbalimbali Huku Serikali Kuu Inachangia Fedha Kwenye Shule Hiyo Kwaajili Ya Kutekeleza
Miradi Mbalimbali Ikiwemo Ujenzi Wa Vyoo Na Miundombinu Mingine Ambapo Kuhusu
Ukubwa Wa Ada Inayotozwa Katika Shule Hiyo Amesema Kila Mwanafunzi Anachangia
Shilingi Elfu 20 Tu.
Mbali Na Hayo Wananchi Wa Kijiji Hicho Pia Wamelalamikia Uongozi Wa Serikali Ya Kijiji
Chao Kwa Kuwanyanyasa Na Kuwadharirisha Kwa Kuwapatia Adhabu Za Kuwapiga Na
Virugu Na Kuwamwagia Maji Wakiwa Kwenye Rokapu Kwa Madai Wameshindwa Kuchangia
Michango Ya Kijiji Na Shule Ya Sekondari Anne Makinda.
Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Ihanga
Wamesema Kuwa Hatua Ya Uongozi Wa Kijiji Kufumbia Macha Wajumbe Na Askali Mgambo
Ambao Wamekuwa Wakiwakamata Baadhi Ya Wananchi Na Kuwadhalilisha Kwa Kuchana
Nguo Zao Na Kuwalaza Chumba Kilichomwagiwa Maji Ni Cha Udhalilishaji Kwao.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Kitendo Cha Askali Mgambo Wakishirikiana Na Baadhi Ya
Wajumbe Wa Serikali Ya Kijiji Hicho Kuwavua Ngua Kwenye Ofisi Ya Serikali Ya Kijiji Ni Cha
Udharirishaji Na Cha Kukiuka Haki Za Binadamu Jambo Ambalo Limewalazimu Kuiomba
Serikali Na Wanasheria Mbalimbali Kuwasaidia Kutatua Tatizo Hilo.
Wakijibu Malalamiko Ya Wananchi Wa Kijiji Hicho Ya Kunyanyaswa Na Kudhalilishwa Kwa
Kuvuliwa Nguo Wakiwa Rokapu Ndogo Ya Kijiji Hicho Uongozi Wa Kijiji Hicho Akiwemo Afisa
Mtendaji Adelhard Mlowe Wamekanusha Kuwafanyia Vitendo Vya Unyanyasaji Wananchi
Wao Na Kusema Kuwa Wao Hutoa Adhabu Kwa Kufuata Kanuni Na Sheria Zilizowekwa.
Wamesema Baadhi Ya Wananchi Wasiyochangia Michango Kwa Wakati Uongozi Hulazimika
Kuwaita Ofisini Na Kufanya Mazungumzo Nao Lakini Wale Wanaokaidi Agizo La Serikali Ya
Kijiji Ndio Wanatumiwa Askali Mgambo Na Baadhi Ya Wajumbe Lakini Hawajashuhudia
Kuwepo Vitendo Vya Unyanyasaji Vinavyofanywa Na Askali Mgambo Wa Kijiji Hicho.
No comments:
Post a Comment