TIMUATIMUA YATUA KWA KIGOGO WA MNADA WA PUGU,MWIGULU ASHIRIKIANA NA MAWAZIRI 3 KUTATUA KERO MACHINJIO YA PUGU
Mh:Mwigulu
Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti
kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili
wadau wa machinjio hayo.
Mwigulu
Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene
wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau
wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.
Mawaziri
kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni
Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana
jambo.
Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjioya Vingunguti.
Mh:Simbachawene
akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini
kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti
kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu
inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa
mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.
Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.
Furaha
ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za
awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya
kukubali hatua alizochukua.
……………………………………………………………………………………………………………………………………….
Ile
kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa
Mh:Rais John Pombe Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu
kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero
zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja
mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu
Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika
machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru
unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha
ya Machinjio hayo.
Hii
leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye
machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni
Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa
na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu
Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar
24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia
sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara
ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu
Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye
eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la
machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu
Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo
lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali
lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati
huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa
machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake
wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
Simbachawene
ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka
kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu
wanaotumia machinjio hayo.
Kwa
upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari
wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo
itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio
hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima
watu hao.
Picha/Maelezo na Festo Sanga
No comments:
Post a Comment