MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG ITUNDUMA KATA YA MTWANGO WILAYA YA NJOMBE ZAKAYO MBOKA AKITOA INJILI KATIKA KANISA LA TAG MELINZE
WAUMINI WA KANISA LA TAG WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA NENO LA YZIMA KANISANI HAPO
MCHUNGAJI ZAKAYO MBOKA ANAHUBIRI NENO
WAUIMBAJI WA KWAYA YA KUTOKA MTWANGO
MUIMBAJI BINAFSI
SAMWELI TWEVE KIJANA HUYO ANAYEONEKANA AMETANUA MIGUU KWA FRAHA AKICHEZA PAMOJA NA WAIMBAJI WENGINE WAKIWA KANISANI HAPO
MUIMBAJI BINAFSI HENRY DANFORD MHEMA AKIWAPAGAWISHA WAUMINI NA NYIMBO ZAKE ZILIZOPO KWENYE ALBAM YAKE YA MAPITO
WACHUNGAJI HAO WANAWAOMBEA WENYE SHIDA MBALIMBALI KANISANI HAPO
MAPEPO WANAONDOLEWA KWA WENYE SHIDA MBALIMBALI
Waumini Wa Kanisa La TAG Wilaya Ya Njombe Wametakiwa Kwenda Kuuanza Mwaka Mpya Kwa Kuongeza Jitihada Mbalimbali Za Kilimo Cha Kibiashara Na Kushiriki Shughuri Za Ufugaji Wa Kuku Na Mifugo Mingine Ili Kukuza Uchumi Wao Na Kuleta Manufaa Kwa Waumini Wa Kanisa Hilo.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mchungaji Wa Kanisa La Tanzania Assembles Of God Lililopo Mtaa Wa Melinze Cefania Tweve Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Mara Baada Ya Ibada Ya Jumapili Iliyofanyika Kanisani Hapo Na Kusema Kuwa Kanisa Linafrahi Kuona Waumini Wanakuwa Na Uchumi Mzuri Na Kufanikisha Kuwasomesha Watoto Wao.
Aidha Mchungaji Tweve Amesema Ujasiliamali Unawasaidia Wakristo Kulitangaza Jina La Mungu Tofauti Na Wakiwa Hawana Shughuli Za Kuinua Uchumi Wao Wengine Wanaweza Kujihusisha Na Swala La Ulevi ,Ujambazi Na Wengine Kushindwa Kuwasomesha Watoto Wao Jambo Ambalo Biblia Inakataza Tabia Hizo.
Kwa Upande Wake Mchungaji Wa Kutoka Kanisa La TAG Itunduma Kijiji Cha Wangama Kata Ya Mtwango Zakayo Ngoga Amesisitiza Wakristo Kudumisha Matendo Mema Kwa Jamii Mbalimbali Ambako Wanaishi Ili Wawe Barua Na Mwanga Kwa Watanzania Katika Kulihubiri Neno La Kristo Huku Akikemea Tabia Za Ukahaba Kuwa Siyo Mapenzi Ya Mungu.
Mchungaji Ngoga Amesema Kumaliza Mwaka Isiwe Fursa Kwa Wakrito Kuruhusu Maovu Kufanyika Katika Jamii Badala Yake Wakemee Tabia Ovu Katika Maeneo Wanayoishi Kwa Kutoa Taarifa Za Uharifu Sehemu Husika Ili Kuishi Kwa Amani Na Utulivu Nakwamba Kipindi Hiki Maadili Kwa Vijana Yameshuka Ambapo Inapaswa Kukemewa Na Watumishi Wa Dini Na Serikali.
No comments:
Post a Comment