Rangers kushuka dimbani kesho
Mwandishi Wetu
LIGI Daraja la kwanza inaendelea
kesho kwa michezo miwili huku timu ya Friends Rangers ikishuka kwenye
Uwanja wa mabatini Mlandizi kuvaana na timu ya KMC.
Ofisa Habari wa klabu ya Friends
Rangers, Asha Kigundula, alisema kuwa wanatambua ugumu wa mechi hiyo
lakini lengo lao ni kushinda na kupata pointi tatu.
Kigundula alisema anatambua kama
wapinzani wao wamejipanga kushinda, lakini nao wapo kwa lengo la kufanya
vizuri na kuondoka na pointi tatu.
Alisema wao hawajataka tamaa wana amini bado wana nafasi ya kupigania kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao.
“Mechi ngumu sana lakini
tumejipanga kushinda mchezo wetu huu, tunatambua uzuri wa KMC lakini
nasi tuko vizuri kama tulivyowatoa kwenye michuano ya FA Cup.
Alisema kuwa wapo katika nafasi nzuri ya kupigana na kufanikiwa kuvuka vizingiti wanavyowekewa na baadhi ya wadau wengi.
Wakati huo huo mechi nyingine ya
ligi hiyo itakuwa kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United mchezo
utakaochezwa kwenye uwanja wa Karume.
No comments:
Post a Comment