SHUGHULI ZA UOKOAJI ZINAMALIZIKA NA SASA WAFANYAKAZI WANAKWENDA KUENDELEA NA MAJUKUMU YAO HUKU WENGINE WAKIAMBIWA WARUDI NYUMBANI HADI KIWANDA HICHO KITAKAPOPONA
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KUSINI EDWARD FRANZ MWALONGO AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA MFANYAKAZI WA KIWANDA CHA TANWAT AKIWA KIWANDANI HAPO
AFISA UTAWALA WA KAMPUNI YA TANWAT EDMUND MUNUBI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA HASARA NA TUKIO ZIMA LA KUUNGUA KWA KIWANDA CHA TANWAT
GARI LA ZIMA MOTO NA UKOAJI MKOA WA NJOMBE LIKIWA ENEO LA TUKIO KWAAJILI YA KUZIMISHA MOTO ULIOKUWEPO KWENYE KIWNADA HICHO
HUKU WALIFANIKIWA KUZUIA MOTO USIFIKE NA KUOKOA MALI ZA KIWANDA HICHO
HUKU NDIKO KULIKOOKOLEWA KUSIUNGUWE
MTANGAZAJI WA UPLANDS FM EMMANUEL SKAWA AKISALIMIANA NA MBUNGE WAKATI ANAWASILI KIWANDANI HAPO
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KUSINI EDWARD MWALONGO AKITEMBELEA ENEO LILILOUNGUA LA KIWANDA CHA TANWAT MJINI NJOMBE
HUU NI MTAMBO ULIOSABABISHA KUTOKEA KWA MOTO HUO BAADA YA KUGONGA BOMBA LA MAFUTA UNAOITWA FOCAL LIFT KWA MUJIBU YA MAJIBU YA LUGHA YA KITAALAMU KIWANDANI HAPO
RANGI ZA UKUTA ZILIZOWEKWA KWENYE BATI HIZO ZIMEKWAJUKA BAADA YA KUPATA JOTO LA MOTO MKUBWA NDANI YA KIWANDA
Kampuni Ya Tanwat Mjini Njombe Imelazimika Kuwasimamisha Kazi Wafanyakazi Mia 190 Waliokuwa Wakifanya Kazi Kwenye Kiwanda Cha Play Wood Kufuatia Kiwanda Hicho Kuteketea Kwa Moto Na Kusababisha Hasara Ya Takribani Bilioni Moja Tukio Ambalo Limetokea Majira Ya Saa Tisa Usiku Wa jana.
Akizungumza Na Uplands Fm Afisa Utawala Wa Kampuni Ya Tanwat Edmund Munubi Amesema Hatua Ya Kuwasimamisha Wafanyakazi Hao Kwa Muda Usiyojulikana Imetokana Na Kuungua Moto Kiwanda Cha Play Wood Ambapo Wakati Jitihada Za Kufanya Tathmini Ya Mali Zilizoungua Wamelazimika Kuwasimamisha Kwa Muda Hadi Kiwanda Hicho Kitakapo Tengenezwa.
Mnubi Amesema Kuungua Kwa Kiwanda Hicho Katika Eneo La Boila Litokea Baada Ya Dereva Aliyekuwa Akiendesha Mashine Ya Kubebea Mizigo Kurudisha Nyuma Mashine Hiyo Na Kugonga Bomba La Mafuta Na Kusababisha Kutokea Kwa Moto Huo Nakwamba Kwa Maelezo Ya Waliokuwepo Usiku Huo Breki Zilikatika Kwenye Mashine Na Kutokea Tukio Hilo.
Kwa Upande Wake Wafanyakazi Wa Kiwanda Hicho Wameelezea Masikitiko Yao Baada Ya Kuungua Kwa Kiwanda Hicho Na Kuuomba Utawala Wa Kampuni Hiyo Kuwatafutia Nafasi Nyingine Ya Kazi Wakati Wakisubiria Hatima Ya Kiwanda Kilichoungua Ili Waweze Kuendesha Maisha Yao Na Familia Zao.
Mbunge Wa Jimbo La Njombe Kusini Edward Franz Mwalongo Akiwa Kwenye Kiwanda Hicho Ametoa Pole Kwa Wamiliki Wa Kiwanda Hicho Na Wafanyakazi Kutokana Na Uzalishaji Kusimama Na Kupongeza Jeshi La Zima Moto Na Uokoaji Kwa Jitihada Walizofanya Huku Msemaji Wa Jeshi La Zima Moto Na Uokoaji Akiomba Ushirikiano Kuoneshwa Pindi Matukio Kama Hayo Yanapotokea.
No comments:
Post a Comment