VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA JKT WATAKIWA KUACHANA NA VITENDO VYA UHARIFU NA WAWE WAZALENDO NA NCHI YAO
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA DESEMBA 29
VIJANA hapa nchini
wanaomaliza mafunzo ya awali ya kujitolea ya jeshi la kejenga Taifa
(JKT) yanayofahamika kwa jina la Operesheni Kikwete wametakiwa
kutojihusiha kabisa na vitendo vya uharifu wa kutumia siraha na badala
yake sasa kupitia mafunzo waliyoyapaya ya kijeshi kuwa
wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na sio vinginevyo.
wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na sio vinginevyo.
Hayo yamesemwa na Bligadia
General Francia Njau kutoka JKT Makao makuu wakati wa sherehe za
ufungaji wa mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea Francis Njau
yaliyofanyika katika viwanja cha mabatibini mlandizi katika kikosi cha
jeshi 832.
Bligadia Njau amesema kwamba
anatambua vijana hao wamejitolea katika kupata mafunzo mbali mbali hivyo
wanapaswa mafunzo hayo waliyoyapata wayatumia vizuri na kuwasisitiza
kutoitumia vibaya kauli mbiu ya Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli
inayosema hapa kazi tu kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
Aidha Njau aliwataka vijana hao
kutokuwa na fikra potofu ya pindi wanapomaliza kuhitimu mafunzo hayo ya
awali wanakwenda kupata ajira na kuwaomba wajitahidi kadri ya uwezo wao
kutumia mafunzo ya waliyoyapata ya ujasirialiamali na ufundi stadi
kama fursa za kuweza kujiajiri wao wenyewe kuliko kuitegemea serikali
pekee.
Naye mwakilishi kutoka JKT Mkao
Makuu Luteni Kanali Piace Kapello amesema kwamba jukumu kubwa la jeshi
la kujenga Taifa ni kuhakikisha inatoa mafunzo na malezi bora kwa
vijana ambao wataweza kulilinda Taifa lao liwe katika hali ya
amani,utulivu na usalama.
Kwa upande wao mmoja wa
wahitimu wa mafunzo hayo ambaye alisoma risala kwa mgeni rasmi pamoja na
Mkuu wa kikosi cha 832 JKT Ruvu Luteni Kanali Charles Mbunge walikuwa
na haya ya kusema kuhusina na mafunzo hayo.
MAFUNZO hayo ya awali ya
kujitotolea yanayojulikana kama Operesheni Kikwete wamewajumuisha vijana
wapatao 1187 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania na yamechukua muda
wa miezi sita kwa kujifunza mambo mbali mbai ya ujasiriamai, stadi za
kazi, ufugaji, kilimo, usafi, nidhamu juu ya ulizni na usalama pamoja
na jinsi ya matumizi ya siraha.
No comments:
Post a Comment