Fedha za mkesha wa amani kuokoa vifo vya wajawazito na watoto
Mwenyekiti wa Jumuiya wa
Makanisa ya Pentekoste,(Katikati) ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya
Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alipokuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
Wachungaji mbalimbali wa Makanisa
ya Pentekoste wakiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili ya
kuzungumzia mkesha utakaofanyika Desemba 31
………………………………………………………………………………..
Na Skolastika Tweneshe-Maelezo
Fedha zitakazopatikana katika
Tamasha la mkesha wa kuombea amani nchini zitatumika kuwasaidia watu
wenye mahitaji hasa afya ya mama na mtoto.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya
Tanzania Fellowship Churches (TFC), Ask
ofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
ofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Malassy alisema kwamba, fedha
zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia
nishati ya jua (solar Panels) ili kuwasaidi wamama wajawazito na watoto
wanaozaliwa.
“Kina mama wajawazito na watoto
wanakufa mahospitalini kutokana na kukosa umeme hasa vijijini, hivyo
tumeamua fedha zitakazopatikana mkesha huu tutanunua solar” alisema
Malassy
Aidha Askofu Malassy amewaomba
wananchi kuzidi kumuombea Rais John Magufuli katika kuliongoza Taifa
la Tanzania ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi ambayo tayari
imekubalika ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo alitambulisha
kitabu kiitwacho IJUE SIRI YA AMANI KWA TAIFA ambacho kinauzwa
Sh.5000 amesema kuwa kitabu hicho kina lengo la kuelimisha thamani na
jukumu la watanzania kuilinda Amani bila kujali itikadi za dini, siasa
wala ukabila
Pia ameomba kwa atakaeguswa na
matatizo yanayowakumba wamama wajawazito anaweza kutuma mchango wake
kwa namba zifuatazo 0755202204,0719202204,0684202204.
Mkesha huo ni wa 18 tangu uanze
kufanyika na mwaka huu utafanyika katika Uwanja wa Uhuru usiku wa
tarehe 31 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Awamu ya Tano Mhe. John
Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment