Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, December 19, 2015

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI LA HITIMISHA SEMINA YAKE YA UNUNUZI WA HISA LEO MJINI NJOMBE

 SEMINA YA UNUNUZI WA HISA KWA VYAMA VYA USHIRIKA YAENDELEA HAPA
 HAWA NI WASHIRIKI WA SEMINA HIYO ILIYOSHIRIKISHA MIKOA MITATU LAKINI MMOJA HAUJAHUDHURIA MKOA WA RUVUMA


 KATIBU MTENDAJI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA WILGIS MBOGORO AKITOA SEMINA YA SIKU MOJA ILIYOFANYIKIA NJOMBE MJINI

 WASHIRIKI WA SEMINA  HIYO



 AFISA USHIRIKA NA MRAJIS WA VYAMA VYA USHIRIKA MKOA A NJOMBE EXAUD SAPALI  AKITROA NASAHA  ZA USHIRIKA AKIWA NDIYE  MWENYEJI  KATI YA WASHIRIKI WOTE.
 MWENYEKITI WA NJORUMA MKOA WA NJOMBE CREMENCE MALEKELA AKIZUNGUMZA NAYE NA WASHIRIKI WA SEMINA HIYO.

 AFISA USHIRIKA MANISPAA YA IRINGA BI.ASSA CHUMA  MKOCHA
 THEOFRID  TOLAGA  KATIBU WA USHIRIKA WA UPANGISHAJI NYUMBA MANISPAA YA IRINGA AKIZUNGUMZA MBELE YA WANASEMINA HAO

 AFISA USHIRIKA WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE





 KATIBU MTENDAJI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA WILLIGIS O.MBOGORO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA SEMINA KUMALIZIKA
 Shirikisho La Vyama Vya Ushirika  Nchini  Leo  Limehitimisha  Semina Ya Ufuatiliaji Juu Ya Ununuzi Wa Hisa  Za Jengo La Ushirika Lililopo  Mtaa Wa Mnazi Mmoja Jijini Dar Es  Salaam    Ambayo Imevikutanisha  Vyama Hivyo Kutoka Mikoa Ya Iringa, Njombe Na Ruvuma   Ambayo Imehitimishwa Mjini Njombe.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Mara Baada Ya Kuhitimisha Semina Kwa Vyama Vya Ushirika  Vya Mikoa Hiyo Ya Iringa Njombe Na Luvuma Katibu Mtendaji Wa Shirikisho La Vyama Vya Ushirika Tanzania Willigis O. Mbogoro  Amesema Chimbuko La Uwekezaji Wa Pamoja Ulianzia Mkoa Wa Dodoma Baada Ya Mkutano Wa Ushirika Nchi Nzima Kuweka Azimio La Uwekezaji Wa Pamoja Wa Ushirika.

Aidha Bwana Mbogoro  Amesema Lengo La Kuanzisha  Dhana Ya Uwekezaji Wa Pamoja  Ni Kutaka  Vyama Vyote Vya Ushirika Na Wanachama  Wa Vyama Hivyo Waweze Kunufaika  Baada Ya   Kugundua Kuwa  Mfumo Uliopo Hauwanufaishi Wanachama Na Vyama Vyao Vya Ushirika  Kutokana Na Kutegemea Uwezo Wa  Kimtaji Kutoka Kwenye Taasisi Za Kifedha Na Makampuni Mengine Katika Kutoa  Huduma Za Shirika.

Amesema Wameanzisha Dhana Hiyo Ya Uwekezaji Wa Pamoja   Kwa Kuanzia Na Jengo Hilo La Ushirika   Ambalo Semina Na Mikutano Yake  Ya Kuelimisha Wanachama  Tangu Mwezi Mei  Mwaka Huu  Ili Jengo Hilo Liweze Kumilikiwa Na Wanaushirika Wenyewe  Ambapo Tarehe 31 Mwezi Decemba Wanahitimisha  Zoezi La Ununuzi Wa Hisa Kwa Kila Mwanachama.


Baadhi Ya Washiriki Wa Semina Hiyo   Wameshindwa Kufikia  Malengo Ya Kuhamasisha  Wanachama  Kununua Hisa  Kwa Wingi  Na Kufikia Kiasi Cha  Fedha  Zisizopungua Milioni  Tano Kwa Kila Chama    Kutokana Na  Jiografia Ya Maeneo, Fomu Kuandikwa Kwa Lugha Ya Kingereza Na Kiwango  Kikubwa  Cha Kununulia Hisa Huku Mkoa Wa Iringa Ukifanya Vizuri Katika Ununuaji  Huo.


No comments:

Post a Comment