HAWA NI WAKUU WA SHULE NA MAAFISA ELIMU SEKONDARI NA MSINGI
Jumla ya Wanafunzi 11,594 Waliohitimu Elimu ya Msingi Mwaka Huu Mkoani Njombe Wamechaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwakani ,Huku Idadi ya Ufaulu Ikiongezeka na Kufikia Asilimia 75.65 Ikilinganishwa na Mwaka 2014 Ambapo Ufaulu Ulikuwa Asilimia 66.5
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Mwelekeo wa Matokeo ya Mtihani wa Kuhitimu Darasa la Saba Iliyosomwa Kwenye Kikao cha Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2016, Imeeleza Kuwa Jumla ya Wanafunzi 15,325 Huku Ufaulu Ukiongezeka Kwa Asilimia 9.15 Ambapo Wasichana Wameonekana Kufanya Vizuri.
Akizungumza Wakati wa Kufungua na Kufunga Kikao cha Uchaguzi wa Wanafunzi , Mwenyekiti wa Kikao Hicho Jakson Saitabau Ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Amewaomba Wadau wa Sekta ya Elimu Pamoja na Halmashauri za Mkoani Huo Kuendelea Kushirikiana Katika Kukabiliana na Changamoto Zinazoikabili Sekta Hiyo Ukiwemo Ujenzi wa Maabara .
Aidha Saitabau Amewataka Wazazi na Walezi Ambao Watoto Wao Wamechaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Kuwasili Kwenye Shule Walizopangiwa , Huku Akiwaagiza Maafiasa Elimu wa Halmashauri Zote za Mkoa wa Njombe Kuhakikisha Wanawachukulia Hatua za Kisheria Wazazi Ama Walezi Watakaowazuia Watoto Kujiunga na Masomo.
Katika Matokeo Hayo ya Kuhitimu Elimu ya Msingi Kwa Mwaka Huu Halmashauri ya Mji wa Makambako Imeshika Nafasi ya Kwanza , Ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe Huku Halmashauri ya Ludewa Ikiendelea Kushika Nafasi ya Mwisho.
No comments:
Post a Comment