JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
|
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na
watanzania wote kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo wakristo wote duniani
huadhimisha siku ya kuzaliwa Yesu Kristo, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamesali ibada ya Krismasi katika misa
takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini
Dar es salaam.
Akitoa
salamu za Krismasi baada ya kukaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
la Dar es salaam Mhadhama Kadinali Polycarp Pengo, Rais Magufuli amewatakia
heri watanzania wote katika sikukuu hii ya Krismasi na kuwataka waishi kama
ambayo Yesu Kristo aliishi, na kwa kutekeleza yote ambayo aliyafundisha.
Ametoa
wito kwa watanzania kuishi kwa amani, upendo na Mshikamano huku wakizingatia
kufanya kazi, hasa wakati huu ambapo yeye mwenyewe anahamasisha uchapa kazi kupitia
kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu"
Rais
Magufuli pia amewataka wakristo wote kuungana kuliombea taifa, kuwaombea
viongozi na kuwaombea watanzania wote ili waweze kutimiza majukumu
yanayowakabili.
"Ndugu
waumini wenzangu, mimi ni yuleyule, nipo vilevile na nimekuja hapa kama Mkristo
wa kawaida, muendelee kuliombea taifa hili na mtuombee pia sisi viongozi
wake" Amesisitiza Rais Magufuli
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
25
Desemba, 2015

No comments:
Post a Comment