Thursday, December 10, 2015
SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMEOMBWA KUWAKUMBUKA WAZEE KATIKA HUDUMA ZA KIJAMII IKIWEMO SUALA LA PENSHENI.
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADI ISKAKA MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA NJOMBE NA RUVUMA JUU YA KUHAMASISHA SUALA LA PENSHENI KWA WAZEE
PICHA YA PAMOJA YA WAANDISHI NA BAADHI YA WAZEE WAKIWA NJE YA OFISI YA SHIRIKA LA PADI TANZANIA
Serikali Ya Awamu Ya Tano Imeombwa Kutilia Mkazo Zoezi La Kuwapatia Pensheni Wazee Mbalimbali Nchini Tanzania Pamoja Na Kupewa Mahitaji Muhimu Ili Kuondoa Umasikini Unaowakuta Baadhi Ya Wazee Ambapo Imedaiwa Pensheni Ikitolewa Kwa Makundi Hayo Uchumi Utaongezeka Miongoni Mwa Jamii.
Akizungumza Kwenye Semina Ya Siku Moja Mkurugenzi Wa Shirika La PADI Tanzania Iskaka Msigwa Amesema Endapo Serikali Itayakumbuka Makundi Ya Wazee Kwa Kuwalipa Pensheni Uharifu Utapungua Kutokana Na Makundi Hayo Kuwa Na Jukumu Kubwa La Kulea Watoto Na Kuendeleza Miradi Yao Na Kujipatia Kipato.
Aidha Msigwa Amesema Kuna Umuhimu Kutolewa Pensheni Kwa Wazee Nchini Ili Nao Waweze Kusomesha Watoto, Kupata Huduma Za Matibabu Bure ,Pembejeo Za Ruzuku Na Mahitaji Mengine Muhimu Ambayo Yatawasaidia Kujikwamua Na Hali Ngumu Ya Umasikini Nakwamba Kutolewa Kwa Pensheni Itapunguza Wimbi La Uharifu Pamoja Na Kukuza Uchumi Wa Nchi.
Amesema Wazee Wanatakiwa Kujiunga Vikundi Na Kuunda Mabaraza Yao Ambayo Yatawasaidia Kupata Mikopo Kutoka Serikalini Kwaajili Ya Kuwawezesha Waishi Maisha Mazuri Bila Kujali Alikuwa Mtumishi Ama Ni Mkulima.
Kwa Upande Wake Wazee Walioshiriki Semina Ya Siku Mmoja Mjini Songea Katika Mtaa Unangwa Wameshukuru Shirika La PADI Kwa Kuanzisha Elimu Ya Wazee Juu Ya Kudai Haki Zao Hususani Za Matibabu Bure Ambapo Wazee Wa Mikoa Ya Ruvuma Na Njombe Wamejipanga Kufikisha Ujumbe Wa Kupatiwa Pensheni Siku Ya Kilele Cha Uhuru Na Maadhimisho Mengine Kwa Lengo La Kuifikishia Serikali Ujumbe Huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment