Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, November 14, 2015

WANAWAKE CHADEMA NJOMBE WAMTAKA MBUNGE WA CHADEMA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE KWENDA BUNGENI KUPIGIA KELELE KERO ZA WANA NJOMBE



Wakazi wa Soko Kuu Njombe Mjini Wakishangilia Kumpokea Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mkoa wa Njombe Bi.Lusia Mlowe Leo.


Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wanawake wa CHADEMA Mkoani Njombe  Wamemtaka Mbunge Mteule wa Chama Hicho Viti Maalumu Bi.Lusia Mlowe Kwenda Bungeni Kupigania Haki  na Kero za Wakazi wa Njombe Kutokana na Kuwepo Kwa Matatizo Lukuki Kwa Wananchi.

Wakizungumza   Mara Baada ya Kumpokea Mbunge Huyo Wamesema Kuwa Sasa Wanaamini Matatizo ya Wananchi wa Njombe Yatakwenda Kumpata Msemaji Bungeni Kutokana na Kutokuwa na Mbunge Kupitia Upinzani Ambaye Amekuwa Akiwasemea Wananchi Kwa  Miaka Yote Mkoani Hapa.

Wamesema Changamoto za Maji,Afya Katika Hospitali ya Kibena Pamoja na Mlundikano wa Michango Wanaamini Atakwenda Kuwawakilisha Vyema Ikiwa ni Pamoja na Kuongeza Nguvu Katika Baraza la Madiwani Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Katika Kupambana na  Ufisadi Unaoweza Kujitokeza.
 

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Njombe Bwana Abu Mtamike Amesema Kuwa Kitendo Cha
Kumpata Mbunge Mmoja wa CHADEMA Katika Mkoa wa Njombe Iwe Chachu ya Kwenda Kushughulikia Kero na Changamoto Kwa Wananchi Huku Akiuagiza Uongozi wa Jimbo la Njombe Mjini Kuendesha Mchakato wa Kuwapata Madiwani wa Viti Maalumu Kwa Amani na Utulivu.

Alatanga Nyagawa ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Ambaye Amepongeza Hatua Jitihada Kubwa Zilizofanywa na Wanachama wa CHADEMA Pamoja na Tume Kumteua Bi.Mlowe Kuwawakilishi Wana Njombe na Kwamba Kilio Cha Wananchi wa Njombe Kimekwenda Kusikilizwa Sasa baada  ya Kukosa Viongozi wa CHADEMA Kwa Muda Mrefu.
 

Kwa Upande Wake Mbunge Mteule wa CHADEMA Viti Maalumu Mkoa wa Njombe Bi.Mlowe Amesema Hatawaangusha Wakazi wa Njombe Pindi Atakapokwenda Bungeni Kwani Atahakikisha Anapambana na Matatizo Yaliyopo Kupitia Bunge na Nje ya Bunge Ikiwa ni Pamoja Kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo Zitakazokuwa Kuwa Chini ya Wabunge wa Kuchaguliwa.

Novemba 17 Mwaka Huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Linaanza Rasmi Vikao Vyake Mara Baada ya Kufanyika Kwa Uchaguzi Mkuu Hapo Oktoba 25 Huku Baadhi ya Majimbo

Yakishindwa Kufanya Uchaguzi Kutokana na Sababu Mbalimbali Zikiwemo za Vifo.

No comments:

Post a Comment