Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, November 17, 2015

WAMUUWA MAMA YAO KWA KUTAKA MASHAMBA NJOMBE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amefika Eneo la Tukio Huko Limage Kata ya Yakobi 




Na Gabriel Kilamlya Njombe
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Wanne Wakiwemo Watoto Wake Kwa Tuhuma za Mauaji ya Imakrata Mbuligwe Mwenye Umri wa Miaka 71 Mkazi wa Kijiji Cha Limage Kata ya Yakobi Mkoani Hapa Kwa Kile Kinachoelezwa Kuwa ni Mgogoro wa Ardhi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Wilbroad Mutafungwa Amewataja Watuhumiwa Hao Wanne Ambao  Wametenda Tukio Hilo Novemba 15 Mwaka Huu na Mwili Kuufukia Kwenye Shimo la Choo Cha Jirani na Nyumba Aliyokuwa Akiishi Kwa Kumnyonga Shingo.

Kamanda Mutafungwa Amesema Watu Hao Wengine Walikuwa ni Wafanyakazi wa Marehemu Pamoja na Mtoto wa M
arehemu Kwa Madai ya Kutaka Mashamba Aliyokuwa Akiyamiliki.

No comments:

Post a Comment