Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, November 17, 2015

CHUO CHA UHASIBU (TIA) MBEYA YAFANYA MAHAFALI YA 3. WAHITIMU WAITAKA SERIKALI KUONDOA KIPENGELE CHA UZOEFU KAZINI.


Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (TIA) akitoa risala katika Mahafali ya 13 ya Chuo hicho na Mahafali ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya.


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Chuo cha Uhasibu(TIA) Profesa Isaya Jairo akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi katika mahafari ya 13 ya Chuo hicho yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Kampasi ya Mbeya.

Mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya Chuo cha Uhasibu (TIA), Nyerembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya aliyemwakilisha Waziri wa Fedha katika sherehe hizo akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa na wahitimu.

Mshehereshaji wa Mahafari ya 13 na ya 3 kufanyika katika kampasi ya Mbeya Charles Mwakipesile akiendelea na wajibu wake wa kuongoza sherehe katika viwanja vya Kampasi ya Mbeya



Wahitimu wa TIA wa nyanja mbali mbali wakiwa kwenye muonekano tofauti wakati wakitunukiwa Vyeti vya uhitimu katika mahafali ya 13 yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya

Wahitimu wa Kampasi ya Mbeya wakipita mbele ya mgeni rasmi kushikana naye mikono baada ya kumaliza kuwatunuku vyeti katika hatua tofauti wakati wa mahafali ya 13 na ya 3 kufanyika katika Kampasi ya Mbeya.



Wahitimu wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio katika mahafali ya 13 na ya 3 kufanyika katika Kampasi ya Mbeya

Baadhi ya Wakufunzi na mgeni rasmi wakitoka katika eneo la sherehe baada ya kumalizika na kufungwa rasmi kwa mahafali ya 13 ya Chuo cha Uhasibu (TIA)

Baadhi ya ndugu na jamaa wakifuatilia matukio mbali mbali wakati wa mahafali ya Wanachuo cha Uhasibu Kampasi ya Mbeya


Kikundi cha Ngoma za asili kikitua burudani katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu kampasi ya Mbeya

Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) tawi la Mbeya, wameiomba Serikali ya awamu ya tano kufuta kigezo cha kuwa na uzoefu kazini ndipo uweze kuajiriwa kwenye taasisi na Serikalini ili kuongeza wigo wa fursa za ajira.
Wahitimu hao  1,689 wa ngazi ya cheti, stashahada na stashada ya uzamili  walitoa rai hiyo  kwenye mahali yao ya 13 na ya 3 kufanyika Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya chuoni hapo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa aliyemwakilisha Waziri wa fedha.
Hata hivyo katika ahadi zake wakati akiomba kura kwa watanzania, Rais  Dk. John Magufuli aliwahakikishia wananchi kwamba katika utawala wake atafute kigezo cha uzoefu na badala yake mtu akitoka masomoni aombe na kupewa ajira kulingana na uwezo wake binafsi na sio kuangalia kigezo za uzoefu.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake, mhitimu Elizabeth Swai,  alisema kwa muda wote wanaokuwepo chuoni wanajifunza masomo kwa nadharia na vitendo hivyo wanapomaliza masomo yao wanakuwa na uzoefu wa kutosha wa kufanya kazi.
“Hili suala kigezo cha uzoefu kazini kiondolewe kabisa. ‘Hivi habari eti uwe na uzoefu kazini usiopungua miaka mitatu’ inatukwamisha sana kwanza ajira zenyewe ni ngumu kupatikana halafu vikwazo kibao. Hivyo tunaiomba Serikali ifute kabisa kigezo hiki kwani hapa chuoni tumesoma kwa nadharia na vitendo,” alisema Swai.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha, Profesa Isaya Jairo, alisema  ni aibu kwa taifa kuona vijana wanaomaliza masomo yao katika fani mbalimbali  kuanza kujihusisha kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kanuni za taaluma zao ikiwamo rushwa, udanganyifu na wizi.
Alisema ‘Niwaombe sana, mnatoka hapa mkiwa mmepikwa na mkapikika hivyo basi mkaoneshe na kuleta mabadiliko ya kweli kwenye taasisi mtakazoajiriwa. Msiwe chanzo cha ubadhirifu na wizi, achaneni na tama ya kutaka kutajirika kwa muda mfupi baada ya kuingia sekta fulani kwani hicho sio ndicho mlichofundishwa hapa’.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya, Nyerembe Mnasa aliwataka wahitimu hao kuonesha weledi wao na kuwa chachu ya kuminya mianya yote ya badhirifu katika kazi zao za uhasibu na manunuzi na kuwataka kuongeza nidhamu kwenye matumizi ya fedha za umma.
“Udhaifu na umasikini wa taifa lolote lile upo kwenye kitengo cha usahibu na manunuzi, ambapo wahusika wasipokuwa makini ujue taasisi hiyo lazima iyumbe tu. Hivyo basi nyinyi wahasibu na maofisa wa ugavi na manunuzi hakikisheni manonesha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma,” alisema Nyerembe.
 Na Mbeya Yetu

No comments:

Post a Comment