Tuesday, November 17, 2015
MTALAAM WA TIBA MBADALA ZA ASILI DR. HAJ HUSSEIN MPAPAI AKABIDHI MSAADA WA BATI 20 KWA MJANE WANGING'OMBE
HUYU NI MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA MSIMBAZI AKIZUNGUMZA BAADA YA KUPOKEA MSAADA WA BATI ZA MAMA MJANE
WANANCHI WA KIJIJI CHA MSIMBAZI WAKIMSIKILIZA DR.MPAPAI KWA MSAADA WAKE NA HUDUMA ZA MATIBABU ANAZOZITOA NA HAPA ANAHUTUBIA WANANCHI
DR.HAJI HUSSEIN MPAPAI KUTOKA MKOA WA MOROGORO MJUKUU WA BIBI. KARIMBWANA AKIENDELEZA HUDUMA ZA MATIBABU NCHI NZIMA TAYARI AMEKWISHA TEMBELEA MIKOA 25 NA KOTE ANATOA HUDUMA ZA MATIBABU NA MISAADA MBALIMBALI KWA WASIYOJIWEZA.
HUYU NDIYE DR. HAJI HUSSEIN MPAPAI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MSIMBAZI KATA YA UHAMBULE
DR. HUYU SASA YUPO NJOMBE NAMBA ZAKE HIZO KWENYE GARI
Wananchi Wa Kijiji Cha Msimanzi Kata Ya Uhambule Wametakiwa Kutunza Mazingira Kwa Kuzingatia Swala La Usafi Na Upandaji Wa Miti Kwa Wingi Ili Kuondokana Na Tatizo La Miripuko Ya Magonjwa Ya Kipindupindu Na Kuhara Yatokanayo Na Uchafu Wa Mazingira Ambayo Yanakemewa Na Serikali Nchini Kote.
Akiongea Na Wakazi Wa Kijiji Cha Msimbazi Wakati Wa Kukabidhi Msaada Wa Bati 20 Mwishoni Mwa Wiki Iliyopita Mtaalamu Wa Tiba Mbadala Za Asili Dr.Haji Hussein Mpapai Amesema Endapo Wananchi Watatunza Mazingira Kwa Ufasaha Itasaidia Afya Za Watanzania Kuboreshwa Kwa Kupata Tiba Zenye Uhakika Kutokana Na Kuwepo Kwa Miti Ambayo Ni Dawa.
Amesema Kuwa Wakati Tanzania Ikiwa Kwenye Wiki La Afya Na Usafi Wa Mazingira Wananchi Wanatakiwa Kutambua Umuhimu Wa Kuunga Mkono Jitihada Hizo Za Serikali Za Kuwakumbusha Wananchi Kujali Mazingira Na Afya Zao Nakwamba Kila Kitu Kinapatikana Kwenye Mazingira Wanayoishi Ikiwemo Dawa Za Asili Pamoja Na Huduma Za Maji.
Katika Hatua Nyingine Dr. Mpapai Amesema Wananchi Wanatakiwa Kuondoa Imani Potofu Za Kishirikina Ambazo Zinasababisha Mauaji Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Yaani Albino Na Vikongwe Kwa Lengo La Kupata Utajili Imani Ambazo Zinaendekezwa Na Baadhi Ya Waganga Wa Jadi Ambao Ni Matapeli Na Hivyo Wananchi Wanapaswa Kuwa Makini.
Kwa Upande Wao Wananchi Wa Kijiji Cha Msimanzi Kata Ya Uhambule Wilayani Wanging'ombe Wamepongeza Taasisi Za Kidini Na Wadau Mbalimbali Ambao Wamemusaidia Mama Mujane Mkazi Wa Kijiji Hicho Akiwemo Dr Mpapai Na Kanisa La Kiluthel Tanzania Usharika Wa Uhambule Kwa Kujitoa Kusaidia Msaada Wao.
DR.Mpapai Amekabidhi msaada wa Bati 20 Katika Kijiji Cha Msimbazi Kata Ya Uhambule Wilaya Ya Wanging'ombe Kwa Mama Aliyeunguliwa Nyumba Yake Na Kupoteza Mume Na Mtoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment