Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya
kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya
kumsikitisha.
“ Rais amesikitishwa na
kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia
amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya
kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa
kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili
sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya
kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”. Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kwenye wodi ya
sewahaji, kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam
leo wakati wa ziara yake ya kushtukiza .
Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye
ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.
Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa
shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati
wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.
Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi
amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha
kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote
vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).
Balozi Sefue pia metumia nafasi hii
kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha
wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.
“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
No comments:
Post a Comment