Bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na kamanda
Ras Makunja juzi jumamosi ya 7 November 2015 walifanikiwa tena kwa mara
nyingine kukonga nyoyo za washabiki mjini Bremen Ujerumani katika
onyesho la kusherekea miaka 10 ya Pan African Org
lililofanyika katika ukumbi wa
Bugerhaus Weserterasse.Kikosi kazi kazi hiko cha FFU-ughaibuni kikiwa na
madansa wao wawili Jessicha Ouyah na Sara Fina waliweza kulimudu jukwaa
na kuwadatisha akili washabiki.
Ngoma Africa band ipo katika
medani ya muziki kwa takribani miaka 22 sasa na kuweka rekodi ya bendi
pekee ya kiafrika barani ulaya inayodumu muda mrefu na kuwanasa
washabiki wa kimataifa.
wasikilize at www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment