Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akimjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadam,Bi
Hellen Kijo Bisimba aliyelazwa hospital ya Agakhan mapema leo kufuatia
ajali ya gari aliyoipata mwishoni mwa wiki barabara ya Al-Hassan Mwinyi
jijini Dar, Dkt Magufuli pia amefanya ziara ya kushtukiza katika
hopsitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwemo pia alitembelea wodi mbalimbali
za wagonjwa na kuwajulia hali zao.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kushtukiza
aliyoifanya Novemba 9, 2015
Rais
Dkt.john Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa moyo wauguzi katika hospitali ya
taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya ghafa kujionea hali halisi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwajulia hali
wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara
ya kushtukiza hospitalini hap oleo na kuwafariji wagonjwa.
Rais akiagana na wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya taifa Muhimbili
Rais akipungia mkono, wagonjwa na wananchi wakati alipotembelea hospitali ya taifa Muhimbili
PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG
No comments:
Post a Comment