Saturday, July 18, 2015
SERIKALI YA KIJIJI CHA MATIGANJORA WILAYANI NOMBE YALALAMIKIWA KUWATOZA WANANCHI MICHANGO ISIYO NA STAKABADHI
Wananchi Na Baadhi Ya Wajumbe Wa Serikali Ya Kijiji Cha Matiganjora Wamelalamikia Kutozwa Michango Pasipo Kupewa Na Stakabadhi Kutoka Kwenye Ofisi Hiyo.
Wakizungumza Na Uplands Fm Kijijini Hapo Wananchi Hao Wamesema Hawana Imani Na Utendaji Wa Mwenyekiti Wao Kutokana Na Kuingilia Majukumu Ya Mtendaji Wa Kijiji Hicho Ikiwemo Ukusanyaji Wa Michango Pamoja Na Kutoa Stakabadhi Kwa Waliochangia.
Aidha Wananchi Hao Wametaka Mwenyekiti Huyo Kuzingatia Taratibu Za Ofisi Yake Ikiwemo Kukasimu Madaraka Kwa Viongozi Waliowekwa Kisheria Ili Kutunza Maadili Ya Uongozi Na Nyaraka Za Serikali.
Akijibia Malalamiko Ya Wananchi Mwenyekiti Wa Kijiji Cha Matiganjora Bwana Ernest Nzilano Amekanusha Malalamiko Yote Yanayotolewa Dhidi Yake Na Kusema Kuwa Kuna Baadhi Ya Wajumbe Hawamtakii Mema Katika Utendaji Wake Wa Kazi Jambo Linalosababisha Kuibuka Kwa Matabaka Miongoni Mwa Wajumbe Wa Serikali Yake.
Bwana Nzilano Amesema Kuwa Kitendo Cha Wananchi Na Baadhi Ya Wajumbe Kutokuwa Na Imani Naye Kimetokana Na Mwenyekiti Huyo Kuzuia Biashara Za Pombe Ambazo Zimekuwa Zikifanyika Asubuhi Hadi Saa Sita Usiku Pamoja Na Kupinga Uchezaji Wa Kamali Kwa Vijana.
Kaimu Afisa Mtendaji Wa Kijiji Hicho Bwana Augustino Mbegalo Amekili Kuwepo Kwa Malalamiko Ya Wananchi Dhidi Ya Mwenyekiti Wao Ambayo Yamesababisha Kutoelewana Miongoni Mwa Viongozi Wa Serikali Na Kuibua Makundi Kati Yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment