Wakati Serikali Ikikemea Jamii Kuepukana Na Vitendo Vya Ukatili Na Unyanyasaji Dhidi Ya Watoto Nchini Bado Vitendo Hivyo Vinaonekana Kuendelea Kujitokeza Kwa Baadhi Ya Maeneo Mbalimbali Ikiwemo Mkoa Wa Njombe.
Hali Hiyo Imejitokeza Kwa Mama Mmoja Neema Kihaka Mkazi Wa Mtaa Wa Kambarage Eneo La Igereke Mjini Njombe Baada Ya Majirani Zake Kumbaini Mama Huyo Akimfanyia Vitendo Vya Ukatili Mtoto Sophia Kinyamagoha Mwenye Umri Wa Miaka 8 Ambaye Ni Yatima.
Wakizungumza Na Uplands Radio Wakiwa Kwenye Ofisi Ya Serikali Ya Mtaa Wa Kambarage Majirani Hao Wamesema Wamelazimika Kumfikisha Ofisini Hapo Baada Ya Kuona Mtoto Huyo Anafanyiwa Vitendo Vya Ukatili Na Unyanyasaji Dhidi Ya Mtoto Huyo Licha Ya Serikali Kukemea Vitendo Hivyo.
Akizungumzia Tuhuma Zinazomkabili Bi.Neema Kihaka Ambaye Ni Mlezi Wa Mtoto Huyo Amekili Kumufanyia Vitendo Vya Unyanyasaji Na Ukatili Mtoto Sophia Kinyamagoha Kwa Kumpiga Na Kumujeruhi Sehemu Za Kichwani Pamoja Kumutumikisha Kazi Ngumu.
Kwa Upande Wao Viongozi Wa Serikali Ya Mtaa Wa Kambarage Akiwemo Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Huo Bwana Braison Mgaya Na Afisa Mtendaji Elia Chilatu Wamethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Na Kuahidi Kuchukua Hatua Kali Za Kisheria Dhidi Ya Mama Huyo Ili Iwe Fundisho Kwa Watu Wengine.
Serikali Kupitia Wizara Ya Maendeleo Ya Jamii Imekuwa Ikisisitiza Jamii Nchini Kuzingatia Haki Za Watoto Ikiwemo Kuwapatia Elimu,Malazi Na Mahitaji Mbalimbali Ya Msingi.
No comments:
Post a Comment