

Timu ya Kupokea Mwenge Wilaya ya Makete
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Fredrick Mwakalebela Akiwa na Mwenge wa Uhuru Leo Asubuhi Katika Viwanja Vya Mang'oto Wilayani Makete Wakati Akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Hiyo.
Picha na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe
Jumla ya Watu Sita Walioshiriki Katika Kupima Wakati wa Mkesha wa Mwenge wa Uhuru Katika Kijiji Cha Kipengele Wilayani Wanging'ombe Wamebainika Kuwa na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Kati ya 145.
Taarifa Ya Idara ya Afya Iliyosomwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Edward Manga Imeeleza Kuwa Kati Ya Watu Hao Sita,Watano ni Wanaume na Mmoja ni Mwanamke.
Kutokana na Takwimu Hiyo Amesema Mapambano Dhidi ya Maradhi ya Ukimwi Yanatakiwa Kuendelezwa Kwa Kila Mmoja Wetu Ili Kutokomeza Janga Hilo Hatari.
Akitoa Ujumbe wa Mwenge Kwa Mwaka 2015 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Huo Bwana Juma Khatibu Chum Amewataka Wananchi Kuendelea Kujitokeza Kupima Katika Vituo Vilivyopo Katika Maeneo Yao Ili Kujua Afya Zao na
Kupanga Maendeleo ya Baadaye.
Pia Amelaani Vikali Wale Wanaobainika Kuwa na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na Kisha Kuamua Kusambaza Kwa Wengine Kwa Makusudi na Kwamba Kitendo Hicho ni Laana Kwa Mwenyezi Mungu.
Mwenge wa Uhuru Umehitimisha Ziara Yake Wilayani Wanging'ombe Kwa Kupitia Miradi Nane Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 534.9 na Kisha Kuukabidhi Wilayani Makete Kabla ya Kuukabidhi Mkoa wa Mbeya Hapo Kesho.
No comments:
Post a Comment