Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, June 30, 2015


RC NJOMBE- AZITAKA HALMASHAURI KUTOA USHIRIKIANO KWA BENKI YA NJOCOBA


 Wa Kwanza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wananchi Njombe[NJOCOBA]Bwana Michael Ngwira Akiwa Kwenye Kikao Cha Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki Hiyo Leo
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Akizungumza Katika Mkutano Mkuu wa NJOCOBA wa Wanahisa

 Baadhi ya Wanachama Wakijisajiri na Wengine Wakinunua Hisa Leo
 Wanachama na Wanahisa wa NJOCOBA
 Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Mikopo Katika Benki ya Wananchi Njombe NJOCOBA na Afisa Mikopo Bwana Danford Mfikwa Akisikiliza Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe 
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Akizungumza na Wanahisa Katika Benki ya Wananchi Njombe NJOCOBA Katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka.

 Baadhi ya Maafisa wa Waandamizi wa Benki ya NJOCOBA

 Baadhi ya Wanachama na Wanahisa wa NJOCOBA Wakiwa Kwenye Ukumbi wa Turbo Kwa ajili ya Mkutano Mkuu

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NJOCOBA Bi.Yohana Kalinga Akizungumza Mara Baada ya Mkuu wa Mkoa Kuhutubia Wanachama wa NJOCOBA

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Amemuagiza Katibu Tawala Mkoa Kuhakikisha Anazifuatilia Halmashauri Ambazo Zinaonekana Kushindwa Kutoa Ushirikiano Katika Benki ya Wananchi Njombe NJOCOBA.

Agizo Hilo Amelitoa Leo Katika Mkutano Mkuu wa  Nne wa Wanahisa wa Benki ya NJOCOBA Akiwa Mgeni Rasmi Ambapo Amesema Kama Kuna Halmashauri Itashindwa Kutoa Ushirikiano Katika Benki Hiyo Basi Haifai Kukuza Uchumi Kwa Wakazi wa Mkoa na Taifa Kwa Ujumla.

Aidha Pia Amesema Kitendo Cha Mwanachama wa Benki Hiyo Kujiingiza Kuchukua Mikopo Kwa ajili ya Masuala ya Starehe Kama Harusi na Kitchen Party Badala ya Malengo Ya Kibiashara ni Kusababisha Kudodoro Kwa Maendeleo ya Benki.

Awali akitoa taarifa fupi ya Bank hiyo makamu mwenyekiti wa bodi ya wanahisa Yohanna Kalinga amezitaja changamoto zinazoikabili banki hiyo kuwa ni pamoja na 
mtaji mdogo kiasi ambacho kinawawia vigumu kuwahudumia wananchi kwa kiwango walichojiwekea.

Kalinga amewaomba wakurugenzi na wananchi kuendelea kuitumia banki ya NJOCOBA na kununua Hisa ili kuiwezesha Bank hiyo kuwahudumia wananchi kwa kadri ya mahitaji yao.

Hata Hivyo Uhaba wa Fedha Katika Benki Hiyo Umesababisha Kushindwa Kununuliwa Kwa Gari la Benki Hiyo Kadri ya Maazimio ya Mkutano wa Mwaka Jana

No comments:

Post a Comment