Muungano Wa Wanawake Tanzania Muwata Umewataka Wanawake Kujitokeza Kwa Wingi Katika Kuwania Nafasi Mbalimbali Za Uongozi Na Kuhamasika Kuwainua Baadhi Ya Wanawake Ambao Tayari Wameingia Kwenye Nyadhifa Za Uongozi Katika Ngazi Mbalimbali Ikiwemo Ngazi Ya Jamii Hadi Taifa.
Akizungumza Na Uplands Fm Katibu Wa Muwata Wa Nyanda Za Juu Kusini Bi.Rebeka Mbonile Amepongeza Wanawake Wa Mkoa Wa Njombe Kwa Kujitokeza Kuwania Nafasi Mbalimbali Za Uongozi Nakuta Jitihada Hizo Kuendelea Ili Kujenga Usawa Wa Maendeleo Kwa Jamii.
Aidha Bi.Mbonile Amesema Kuwa MUWATA Umelazimika Kutembelea Maeneo Mbalimbali Za Nyanda Za Juu Kusini Ili Kuhamasisha Wanawake Kutambua Umuhimu Wao Kutokana Na Muamuko Wa Wanawake Kuwa Mdogo Kwa Nyanja Mbalimbali Kiuchumi Na Hata Kuomba Uongozi Ngazi Ya Jamii.
Bi.Mbonile Amesema Kuwa Watanzania Wanatakiwa Kudumisha Amani Na Utulivu Katika Jamii Kwa Kwa Kuzuia Maovu Yasiendelee Katika Kipindi Hiki Ambacho Tunaelekea Kwenye Uchaguzi Mkuu Huku Mwanamke Akidaiwa Kuwa Ndicho Chombo Kitakacho Saidia Kutokomeza Uharifu Katika Jamii.
Kayemba Mpeleka Ni Mshauri Wa Mujata Kanda Ya Kusini Ambaye Amesema Kuwa Hatua Ya Katibu Wa MUWATA Nyanda Za Kusini Kutembelea Wananchi Wa Mikoa Mbalimbali Ya Kusini Ni Kuwahamasisha Wanawake Kuchukua Hatua Zitakazo Kubalika Kisheria Endapo Atahujumiwa Kwenye Uchaguzi Na Kukataa Kushiriki Maandamano Yanayoweza Kusababisha Vurugu.
Awali Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Wajumbe Wa Mujata Mkoa Wa Njombe Wamepongeza Asasi Hiyo Ya Mujata Kwa Kuwaunganisha Na Kujadili Mambo Yanayowahusu Wanawake Na Jamii Kwa Ujumla Ambapo Kupitia Muungano Wa Mujata Maovu Yanaweza Kupungua Andapo Jamii Itaungana Kupambana Na Maovu.
No comments:
Post a Comment