Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, June 8, 2015

MADUKA YA WAFANYABIASHARA YAFUNGWA TENA KESI YA JONSON MINJA MAHAKAMANI TENA LEO






MADUKA YA NJOMBE MJINI YAKIWA YAMEFUNGWA HADI MUDA HUU



 NI KESI YA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA JWT JONSON MINJA IMESABABISHA MADUKA KUFUNGWA

HALI ILIVYO HIVI NJOMBE

 HAPA NI ENEO LA KITUO KIKUU CHA MABASI NJOMBE NAPO WAMEFUNGA BAADHI YA WAFANYABIASHARA



Wakati Taifa la Tanzania Likitarajiwa Kushuhudia Adha Kubwa ya Kufungwa Kwa Maduka Kwa Takribani Nchi Nzima Kwa Muda wa Siku Tatu Kuanzia Leo ,Wananchi Mkoani Njombe Wamewaomba Wafanyabiashara Hao Kuangalia Namna ya Kufungua Maduka Hayo Wakati Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa Ikisikilizwa Mjini Dodoma.

Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya JWT Bwana Johnson Minja Ilipangwa Kusikilizwa Kwa Muda wa Siku Tatu Mfululizo Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Siku Ambazo Wafanyabiashara Watakwenda Kufunga Maduka Yao.

Kituo Hiki Kimezungumza na Baadhi ya Wananchi Mjini Njombe Juu ya Adha Itakayojitokeza Endapo Maduka Hayo Yatafungwa Kwa Siku Zote  Kuanzia Juni Nane Hadi Kumi Mwaka Huu Huku.

Wengine Wamesema  Kuwa ni Vyema Serikali Ikiangalia Namna ya Kutatua Tatizo Hilo Haraka Iwezekanavyo Badala ya Kuendelea Kushuhudia Maduka Yakifungwa Kutokana na Tatizo la Mashine za EFD.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa Johnson Minja Akizungumza na Kituo Hiki Kwa Njia ya Simu Toka Mkoani Dodoma Amesema Kuwa Utaratibu Rasmi Utafahamika Kesho Baada ya Mahakama Kuzungumza Chochote Kama ni Kweli Kesi Hiyo Itakwenda Kwa Siku Zote Tatu Au Itaahirishwa.

Minja Amesema Kuwa Licha ya Kuwepo Kwa Maombi ya Wananchi na Wateja Wao Juu ya Kutofunga Maduka Hayo Lakini Hata Yeye Amekuwa Akiwataka Wafanyabiashara Hao Kufungua Maduka Bila Mafanikio Mbali na Kwamba Hata Wao Wanapata Hasara Kubwa.

No comments:

Post a Comment