Sunday, June 7, 2015
WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA,MIAKA MITANO MTOTO KUSOMA BWENINI HADI CHUO KIKUU MAADILI YA NAHARIBIKA
MTOTO JACKRINE MGAYA AKITOA SOMO LA INJILI KATIKA KANISA LA T.A.G
WALIMU WA WATOTO AKIWEMO HENRY NDONE AKIWA NA MWENZAKE NJE YA KANISA WAKIJADILI BAADA YA IBADA KUMALIZIKA
WATOTO WAKIWA KANISANI PAMOJA NA WAUMINI WENGINE
MAMA MCHUNGAJI TWEVE AKITOA MAELEKEZO KIDOGO
MTOTO JACKRINE MGAYA AKISOMA INJILI MBELE YA MCHUNGAJI TWEVE
waumini hapa wanatoka Baada Ya Ibada Kumalizika
Wazazi Na Walezi Wametakiwa Kutoa Huduma Za Msingi Kwa Watoto Iikiwemo Elimu,Malazi, Huduma Za Kiroho Na Ulinzi Pamoja Na Kuacha Tabia Ya Unyanyasaji Na Ukatili Kwa Watoto Wao Ili Kujenga Taifa Lenye Maadili Ya Kikristo Nchini .
Rai Hiyo Imetolewa Na Mchungaji Wa Kanisa La Tanzania Asembles Of God TAG Lililopo Mtaa Wa Menze Cefania Tweve Wakati Akiongea Na Waumini Wa Kanisa Hilo Katika Ibada Ya Kwanza IKiwa Ni Sikukuu Ya Watoto Nchini Katika Kanisa Hilo Nchini.
Aidha Mchungaji Tweve Amesema Kuwa Wazazi Wanatakiwa Kuepuka Tabia Ya Kupeleka Watoto Kwenda Kuishi Na Ndugu Zao Na Kuwatumikisha Kazi Za Ndani Ambapo Amesema Kuna Baadhi Ya Wazazi Wamekuwa Wakiwatesa Kwa Kuwanyima Chakula Huku Akishaauri Wazazi Kuwaelimisha Na KuWazoesha Katika Shughuli Za Kilimo Kwa Manufaa Yao Ya Baadaye.
Mchungaji Tweve Ametaka Wazazi Kuakagua Wanako Lala Watoto Wao Na Kuweka Mazingira Mazuri Huku Akikemea Vikali Tabia Ya Baadhi Ya Wazazi Kuwapeleka Watoto Wadogo Kuanzia Miaka Mitano Kuishi Bwenini Hadi Chuo Kikuu Kwa Madai Wanakosa Malezi Ya Mama Na Baba Na Kufanya Kuiga Utamaduni Wa Kigeni Ikiwemo Kuvaa Mavazi Yasiostahili.
Katika Neno La Injili Kanisani Hapo Kwa Niaba Ya Watoto Wengine Jackrine Mgaya Amesema Watoto Wanatakiwa Kuwaheshimu Wazazi Ili Waishi Miaka Mingi Na Hri Duniani,Kuwa Na Tabia Njema Kwa Wakubwa Huku Wazazi Nao Wakitakiwa Kuwajali Watoto Na Kuwapatia Heshima Zao Zote.
Akisoma Risala Kwa Niaba Ya Watoto Wote Akiwa Kanisani hapo Musa Chami Amesema Kuwa Watoto Wanaomba Kutengewa Darasa Lao Kuliko Kuchanganyikana Na Wakubwa,Walimu Wao Kutiwa Moyo Hata Kwa Maneno Ya Faraja Kwani Wanawafundisha Vizuri,Viti Vya Kukalia Watoto Havipo,Watoto Wakifundishwa Vizuri Biblia Ndilo Kanisa La Baadaye Huku Wakichangia Shilingi Laki Tano Kwaajili Ya Kumtia Moyo Mchungaji Na Kanisa Zima La T.A.G Melinze.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment