Baadhi
ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama
barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano
cha kikosi cha usalama barabarani
Baadhi
ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama
barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano
cha kikosi cha usalama barabarani
Na Augustus Fungo, Balozi wa Usalama Barabarani
HIVI karibuni imejitokeza njia
mpya ya kusaidia kupambana na wimbi la ajali za barabarani, ambapo
pamoja na faini kwa madereva wanaokiuka sheria za barabarani wamekuwa
wakipigwa picha na baadaye picha hizo kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii
au magazetini na hata wakati mwingine kwenye televisheni. Mathalani
katika mtandao wa facebook kundi la Mabalozi wa Usalama Barabarani
maarufu kama, RSA wakishirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani hutumia mbinu hii kuwapiga picha wakiukaji wa sheria za
barabarani kisha kuzituma katika Kituo cha Mawasiliano cha Usalama
Barabarani (Traffic Control Center, TCC).
Kituo hiki huwatumia picha hizi
ambazo pia ni ushahidi askari waliopo katika vituo mbalimbali
barabarani, ili kuwezesha watuhumiwa kukamatwa na magari husika. Baada
ya kukamatwa magari husika askari humwandikia faini mkosaji, kumpiga
picha na kuituma kwenye kituo cha mawasiliano ya polisi (TCC) ambacho na
chenyewe hutoa mrejesho kwa watoa taarifa. Picha hizo hatimaye kuwekwa
kwenye mtadao wa facebook, hutumika kuandaa vipindi vya televisheni vya
kuelimisha jamii mfano, ni kipindi cha ‘Aibu yako’ kinachorushwa na
televisheni ya ITV na pia picha hizo huhifadhiwa na kikosi cha usalama
barabarani kwa ajili ya kumbukumbu na rejea iwapo dereva husika atarudia
kosa hilo.
Njia hii mpya ambayo inaitwa
kutaja na kuaibisha, ama kwa kiingereza “Naming and Shaming” ni maarufu
sana inayotumika si tu na nchi nyingi za Ulaya bali pia na mashirika ya
haki za binadamu kama ‘Human Rights Watch’, hutumia kuyaaibisha mataifa
yaliyokubuhu kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Saudi Arabia kupitia sheria yake
ya makosa ya mtandao (Anti-cyber-crime law (Royal Decree No. M/17 dated 8
Rabi1 1428) imepitisha mbinu hii kama mojawapo ya adhabu. Mbinu kama
hii hutumika pia katika nchi nyingi za Ulaya kuwaaibisha watu au
makampuni yanayokwepa kodi. Moja ya makampuni yaliyowahi kuathirika na
kadhia hii ni kampuni ya Kahawa ya Starbuck. Januari 15, 2015, serikali
ya Uingereza iliwataja na kuwadhalilisha waajiri 37 wa Uingereza
walioshindwa kulipa kima cha chini kwa wafanyakazi wao.
Hata hivyo, mwandishi James Meernick(2012), anaitaja njia hii kama chaguo kuu la mashirika mengi ya kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa.
Njia hii hutumika ikiaminika kwamba kumuweka mtu au taasisi hadharani ili aweze kujiona mwenyewe, aonwe na familia yake, marafiki zake, na hata waajiri wakati akitenda kosa inasaidia kumfanya mtu ajitafakari na kutorudia kosa au pia kuwafanya wanaomzunguka kumpa shinikizo la kufuata sheria au kuheshimu haki za wengine.
Hata hivyo, mwandishi James Meernick(2012), anaitaja njia hii kama chaguo kuu la mashirika mengi ya kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa.
Njia hii hutumika ikiaminika kwamba kumuweka mtu au taasisi hadharani ili aweze kujiona mwenyewe, aonwe na familia yake, marafiki zake, na hata waajiri wakati akitenda kosa inasaidia kumfanya mtu ajitafakari na kutorudia kosa au pia kuwafanya wanaomzunguka kumpa shinikizo la kufuata sheria au kuheshimu haki za wengine.
Baadhi
ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama
barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano
cha kikosi cha usalama barabarani
Pamoja na hayo baadhi ya wadau
nchini wameipokea mbinu hii kwa hisia tofauti. Wengine wamedai kwamba ni
kinyume cha sheria japokuwa hawajaweka kutaja ni sheria gani hasa
inayokiukwa kwa kufanya hivyo; wengine wamedai ni kuingilia
usiri(privacy) ya mtu bila kusema ni kwa vipi siri ya mtu inaingiliwa
pale anapotenda kosa. Pia wameshindwa kuushawishi umma kuelewa je, mtu
anapokuwa mathalani anatanua barabarani (matumizi mabaya ya barabara),
au analipita gari pasiporuhusiwa au anakimbia kwa zaidi ya mwendo kasi
wa 80 (speed) kinyume na sheria akakamatwa akapigwa picha ni kwa jinsi
gani anadhalilishwa zaidi ya kuaibishwa?
Maana wakati anapigwa hiyo picha
kwanza anakuwa ameshakubali kosa; pili, anakuwa hajavuliwa nguo wala
kurushwa kichurachura, kupigwa au kufungwa pingu. Isitoshe wapinzani wa
mbinu hii wameshindwa kuwashawishi Watanzania kuelewa iwapo kumpiga
picha mkosaji barabarani ni kosa, inakuwaje au ni mara ngapi watuhumiwa
wamekuwa wakipigwa picha wanapofikishwa mahakamani?
Je, ni mara ngapi kumekuwa na
matukio mfano ya ujambazi na watuhumiwa wa ujambazi katika eneo la tukio
au walipokamatwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapiga picha. Je, huku
si kuvunja sheria? Itakumbukwa Kituo cha Luninga cha ITV na vingine
nchini vimewahi kurusha kipindi maalumu kinachoonesha askari wanaodaiwa
wanapokea rushwa, mbona hili halikusemewa? Ni mara ngapi polisi wamekuwa
wakitoa picha wa watu wanaotafutwa kwa uhalifu (wanted), ni mara ngapi
waajiri wamekuwa wakitoa picha za wafanyakazi wao waliofukuzwa kazi kwa
makosa ya kutokuwa waaminifu? Iweje leo picha za wakosaji wa barabarani
tu tutolewa ionekane wanadhalilishwa?
Wapo watu wametoa hoja kuwa dereva
mkosaji ana maisha yake mengine eti yanaathirika kutokana na kupigwa
picha. Kimsingi hoja hii haina mashiko kwakuwa lengo la mbinu ya kutaja
na kuaibisha ni kumfanya muhusika aone aibu kwa upuuzi alioufanya na
kuweza kujirekebisha. Dereva anayejua kuwa hiyo inaweza kumuharibia
hadhi yake huko baadae atakuwa makini zaidi kutokiuka sheria za
barabarani au kuchezea maisha ya watanzania wasio na hakia.
Picha kama hii inaweza kutumwa katika kituo cha cha taarifa cha kikosi cha usalama barabarani kwa hatua zaidi.
Baadhi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani maarufu kama, RSA.
Gari za serikali, mashirika ya
umma, miradi, na zinginezo haziko juu ya sheria. Bila kujali operesheni
wanayofanya au lengo la safari yao hawapaswi kuvunja sheria, na endapo
watakuwa wamevunja sheria kwa sababu ya kwenda kuhudhuria dharula
husika, askari aliyesimamisha hilo gari akiridhika na sababu hiyo hata
toza faini wala kupiga picha, kwa hiyo hakuna kitakachoathirika. Na
endapo kuna hofu ya matumizi mabaya ya hizo picha, atakaye wajibika ni
huyo anayetumia vibaya picha hiyo ili mradi tu picha halisi (original)
ya tukio zima ipo na ndiyo itakayotumika kama ushahidi dhidi ya mtu
aliyeitumia picha vinginevyo.
Ni ushauri wetu kuwa askari
waendelee na mbinu hii ili wavunja sheria waaibike na kuweza
kujirekebisha. Haiwezekani dereva amesomea amejaribiwa na kupewa leseni,
anajua amebeba abiria kwenye gari lake halafu aendeshe kwa mwendo
hatarishi, ayapite magari mengine kana kwamba amebeba viazi, au abiria
ni mateka wake.
Faini peke yake hazi saidii.
Binafsi ningependa hata siku moja mahakama imhukumu mkosaji kufagia
barabara za Kariakoo kwa wiki zima badala ya kumpeleka jela hii
ingesaidia zaidi kurekebisha watu. Kimsingi ipo haja kama taifa tuwe na
adhabu mbadala. Na kwa kuwa hakuna sheria inayovunjwa kwa mtu kupigwa
picha wakati akitenda kosa na kuwekwa hadharani, mbinu hii bado
itaendelea kuwa sahihi ili wahusika waache kutenda makosa ambayo
yanagharimu si tu maisha ya watanzania bali pamoja na uchumi wa nchi.
Naimani Jeshi la Polisi ni Jeshi lenye ueledi na wataalamu mbalimbali
hivyo litaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kurekebisha tabia na
kutekeleza sheria. Hii ndio imani yangu kwa taasisi hii muhimu nchini
Tanzania, wananchi tushirikiane nao.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu sote.
No comments:
Post a Comment