KAMANDA NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Watu Wanne Kwa Tuhuma Za Unyang'anyi Wa Mali Kwa Kutumia Nguvu Katika Tukio Ambalo Limetokea Jana Njiapanda Ya Magereza Baada Ya Kumvamia Na Kumpora Fedha Shilingi Milioni Tano Mfanyabiashara Cecelia Mwalongo Na Kukimbia Na Gari Lao Kuelekea Luvuma.
Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe SACP Fulugence Ngonyani Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa Ni Pamona Na Jumanne Makumbati Mwenye Umri Wa Miaka 40,Joram Gerelota Mwenye Umri Wa Miaka 44,Alfred Stima Warioba Mwenye Umri Wa Miaka 28 Na Chagari Mwenda Wote Wakazi Wa Jijini Dar Es Salaam.
Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Watuhumiwa Hao Walifanya Tukio Hilo Mnamo Februari 2 Majira Ya Saa Sita Na Nusu Wakiwa Na Gari Aina Ya Toyota Lenye Namba Za Usajiri T410 CFQ Rangi Ya Silva Aina Ya Toyota IST Ambalo Limehifadhiwa Kituoni Ambapo Baada Ya Kumvamia Na Kupora Fedha Hizo Na Kisha Kukimbia Kuelekea Barabara Ya Njombe Luvuma.
Amesema Kuwa Watuhumiwa Hao Walikamatwa Baada Ya Ushirikiano Mkubwa Na Wananchi Wa Njombe Na Jeshi La Polisi Hadi Walipofanikiwa Kuwakamata Mpakani Mwa Mkoa Wa Njombe Na Luvuma Ambako Wananchi Waliwasiliana Na Wananchi Wa Luvuma Na Kuweka Vizuizi Barabarani Na Kufanikiwa Kuwakamata.
No comments:
Post a Comment