
KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA YAKE
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amesema Serikali Inaendelea Na Jitihada Za Kuboresha Maeneo Ya Utoaji Haki Ikiwemo Madawati Ya Jinsia Na Hatua Mbalimbali Za Kufikia Mahakama Katika Mashauri Ya Jinai, Rushwa Ambapo Wadau Wa Sheria Nao Wanapaswa Kutii Na Kuheshimu Sheria Za Nchi.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Wakati Wa Siku Ya Sheria Nchini Ambayo Kwa Mkoa Wa Njombe Imefanyika Katika Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Na Kusema Kuwa Haki Inakwenda Na Wajibu Na Wadau Watimize Wajibu Wao Kwa Manufaa Ya Jamii Nzima.
Bi. Dumba Amesema Ujumbe Wa Mwaka Huu Umeelekeza Kwa Wananchi Kutii Sheria Za Nchi,Kuepuka Kutengeneza Jinai Na Uharifu Kwa Lengo La Kudumisha Amani Na Utulivu,Kukabiliana Na Athali Zinazotokana Na Utandawazi Na Mmomonyoka Wa Maadili Kwa Maslahi Ya Kudumisha Mila,Tamaduni Na Desturi Nzuri Zinazojenga Uzarendo Na Umoja Wa Taifa.
Amesema Kuwa Serikali Imekuwa Ikiendelea Na Jitihada Za Kutoa Fursa Ya Uhuru Wa Mahakama Kwa Kuhakikisha Maeneo Yake Yanaboreshwa Ambapo Uboreshaji Wake Utakwenda Awamu Kwa Awamu Kuboresha Mazingira Yake .
Kwa Upande Wake Hakimu Mkazi Mfawidhi Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Augustino Rwezile Amesema Kuwa Mahakama Hiyo Hapo Mwakajana Kulikuwa Na Mashauri YA Muda Mrefu Sabini Na Tano Ambapo Mwaka Huu Wanamashauri Matatu Ambayo Ni Ya Mwaka 2013.
Hakimu Rwezile Amepongeza Jeshi La Polisi Kwa Jitihada Kubwa Zilizofanyika Katika Kipindi Cha Mwaka 2014 Za Kuhakikisha Uchunguzi Wa Mashauri Mbalimbali Unakamilika Ambapo Hali Hiyo Inasaidia Kuondoa Dhana Ya Wananchi Kusema Kesi Ikienda Mahakamani Lazima Rushwa Itolewe Ndipo Haki Itendeke.
Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu Inasema "Fursa Ya Kupata Haki,Mchango Na Wajibu Wa Serikali,Mahakama Na Wadau" Ambapo Kutokana Na Mada Hiyo Inatoa Wasaa Wa Kujadili Mambo Makuu Mawili Ambayo Ni Fursa Ya Kupata Haki, Mchango Na Wajibu Wa Serikali,Mahakama Na Wadau.
No comments:
Post a Comment