Waumini Wakikristo Mkoani Njombe Wameungana Na Wakristo Wengine Nchini Kusheherekea Kuzaliwa Kwa Bwana Yesu Kristo Ambapo Wameombwa Kumuenzi Mungu Kwa Kutenda Mema Katika Sikukuu Ya Krismasi Na Kuwajali Wasiyo Jiweza Na Watoto Yatima Kwa Kuwashirikisha Kwenye Sikukuu Hiyo.
Akizungumza Na Waumini Wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Muhashamu Askofu Alfred Maluma Amesema Wakristo Ni Vema Wakatambua Umuhimu Wa Kutenda Mema Mbele Ya Mungu Na Kwamba Wanapaswa Kusherehekea Sikukuu Ya Krismasi Kwa Amani Na Utulivu Kwani Krismasi Ni Sikukuu Ya Kushangiria Utukufu Wa Ufufuko Wa Kristo Bwana Wetu.
Muhashamu Askofu Maluma Amesema Yesu Amezaliwa Na Kuchukua Sura Ya Binadamu Ili Amufikishe Mwanadamu Kwenye Utukufu Na Kumkomboa Mwanadamu Na Kuishi Kwa Kufuata Yale Yanayompendeza Mungu Kwa Kuepukana Na Matendo Maovu Ikiwemo Ulevi, Wizi,Chuki Na Mauaji Ili Kutozisambaratisha Familia Na Jumuiya Mbalimbali Za Wakristo.
Muhashamu Askofu Maluma Amesema Kuwa Jamii Inatakiwa Kuwatakia Mema Watu Wengine Na Katika Siku Ya Sikukuu Ya Krismasi Inatakiwa
Kushirikiana Na Majirani Na Kuzidisha Upendo Katika Siku Hii Ya Kuzaliwa Kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Wakizungumza Mara Baada Ya Kumalizika Kwa Misa Takatifu Katika Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Wamesema Siku Hii Wameipokea Vizuri Na Kuwaasa Wakristo Wengine Kuhakikisha Hawatendi Matendo Ambayo Yapo Kinyume Na Matendo Ya Mungu Kwani Kutokufanya Hivyo Ni Kumkosea Mungu.
Wamesema Siku Hii Ya Krismasi Wakristo Wanatakiwa Kuwa Makini Na Watoto Wao Na Kuwashirikisha Katika Sherehe Ya Pamaoj Na Vyombo Vya Ulinzi Na Usalaama Kushirikiana Na Wakristo Wengine Kupinga Matendo Mabaya Ambayo Yataweza Kuhatarisha Amani Na Utulivu Katika Jamii.
No comments:
Post a Comment