Sunday, December 28, 2014
SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE MSTAAFU WA JIMBO LA NJOMBE KUSINI PR.NDEMBWELA NGUNANGWA YALIOFANYIKA NJOMBE KIJIJI CHA IGOMA
Spika Wa Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Anna Makinda Leo Ameongoza Maelfu Ya Wakazi Wa Mji Wa Njombe Katika Mazishi Ya Aliyekuwa Mbunge Mstaafu Profesa Ndembwela Ngunangwa Aliyefariki Kwa Ugonjwa Wa Shinikizo La Damu Na Kisu kali.
Akizungumza Kwenye Mazishi Ya Mbunge Mstaafu Wa Jimbo La Njombe Kusini Kupitia CCM Profesa Ngunangwa, Spika Wa Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Anna Semamba Makinda Amesema Marehemu Alikuwa Mfano Wa Kuigwa Wakati Wa Uhai Wake Hususani Kwa Upande Wa Kuhimiza Elimu.
Spika Makinda Amesema Jamii Inatakiwa Kumutumikia Mungu Siku Zote Na Kuweka Mazingira Mazuri Wakati Wakiwa Hai Ambapo Amesema Kuwa Kifo Cha Marehemu Mbunge Mstaafu Profesa Ngunangwa Kimeacha Pengo Kubwa Kwa Watanzania Wote Kutokana Na Ushauri Aliokuwa Akiutoa Enzi Za Uhai Wake.
Spika Makinda Amesema Wakristo Wanawajibu Mkubwa Wa Kuiombea Nchi Yetu Ya Tanzania Ili Kudumisha Amani Na Utulivu Na Kutaka Wakristo Waishi Kwa Kupendana Na Kuondoa Tofauti Zao Kwa Kuiombea Nchi Amani Na Mshikamano.
Akisoma Historia Ya Marehemu Mbunge Mstaafu Wa Jimbo La Njombe Kusini Profesa Ndembwela Ngunangwa ,Mwenyekiti Wa Familia Ya Akina Ngunangwa Bwana Erasmo Ngunangwa Amesema Marehemu Alikuwa Mbunge Wa Jimbo La Njombe Kusini Kuanzia Mwaka 1990 Hadi 1995 Ambapo Kabla Ya Kuwa Mbunge Alihimiza Maendeleo Ya Elimu Ya Sekondari Kwa Kufadhili Shule Za NDDT.
Aidha Bwana Ngunangwa Amesema Marehemu Profesa Ngunangwa Alikuwa Akisumbuliwa Na Maradhi Ya Kisukari Na Shinikizo La Damu Ambapo Alipelekwa Katika Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbile Na Tarehe 23 Mwezi Huu Alifariki Dunia Na Mazishi Yamefanyika Jana Katika Makaburi Ya Kijiji Cha Igoma Kitongoji Cha Itowelo Taarafa Ya Igominyi.
Mazishi Ya Aliyekuwa Mbunge Mstaafu Wa Jimbo La Njombe Kusini Profesa Ndembwela Ngunangwa Umehudhuriwa Na Viongozi Mbalimbali Wa Serikali,Dini Na Wa Kisiasa Ambapo Salamu Mbalimbali Zilitolewa Na Viongozi Hao Akiwemo Padre Wa Kanisa Katholiki Parokia Ya Igoma Aliyeongoza Misa Hiyo Pamoja Na Salamu Za Mkurugenzi Wa Bodi Ya Chama Cha Walimu Wastaafu Mkoa Wa Njombe Mendecki Mhomisoli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment