Mtu Mmoja Anaye dhaniwa Kuwa Ni Askali Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Mahamudu Ndauka Amefariki Dunia Papo Hapo Baada Ya Gari La Polisi Makambako Lenye Namba Za Usajili PT 0766 Aina Ya Deffender Kupinduka Katika Eneo La Makambi Ya Kampuni Ya Tanwat Ya Namba Four Na Kusababisha Kifo Hicho.
Wakizungumza Na Mtandao Huu Wa Michaelngilangwa.blogspot.com Baadhi Ya Mashuhuda Wa Tukio Hilo Wamesema Kuwa Ajali Hiyo Imetokea Decemba 19 Majira Ya Saa Tano Usiku Katika Eneo La Mto Ipang'ira Wakati Gari Hilo Aina Ya Defenda Mali Ya Polisi Makambako Ikielekea Barabara Ya Kupitia Ibumila Kuelekea Kijiji Cha Nyombo.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Kuwa Wameshindwa Kutambua Gari Hilo Lilikuwa Likielekea Wapi Usiku Huo Na Likiendeshwa Kwa Mwendo Kasi Ambapo Kila Mmoja Ameonekana Kuwa Na Mtazamo Tofauti Huku Wengine Wakidhani Huenda Gari Hilo Linatumiwa Kubebea Nyama Za Ng'ombe Wa Wizi Nyakati Za Usiku.
Akizungumza Na Mtandao Huu Kwa Niaba Ya Daktari Mfawidhi Wa Hospitali Ya Kibena Dr. Patrick Msigwa ,Afisa Muuguzi Wa Zamu Katika Hosipitali Ya Mkoa Wa Njombe Ya Kibena Bi. Veronika Mangu Amethibitisha Kupokea Maiti Moja Ya Askali PC Mahamudu Juma Wa Kituo Cha Makambako Ambaye Amefariki Dunia Baada Ya Kupata Ajali Katika Mto Ipang'ira Karibu Na Makambi Ya Kampuni Ya Tanwat Ya Namba 4.
Kwa Upande Wake Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Vifo Vya Watu Wawili Vilivyotokana Na Ajali Za Magari Barabarani Kikiwemo Kifo Cha Askali Wa Polisi Mwenye Namba F 6435 PC Mahamoud Ndauka Aliyefariki Baada Ya Kutokea Kwa Ajali Ya Gari La Polisi Makambako.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Kuwa Askali Huyo Namba F 6435 PC Mahamoud Ndauka Alikuwa Akiendesha Gari Yenye Namba PT 0766 Mali Ya Polisi Makambako Ambapo Baada Ya Kufika Kwenye Mto Ipang'ira Karibu Na Makambi Ya Kampuni Ya Tanwat Ya Namba Four Majira Ya Saa Tano Usiku Iliacha Njia Na Kupinduka Na Kusababisha Kifo Hicho.
Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Tukio Lingine Gari Lenye Namba Za Usajiri T 9311 Aina Ya Toyota Ikiendeshwa Na Anord Mwanyanje Mkazi Wa Dar Es Salaam Mali Ya Julith Kweyambe Ilimgonga Mtembea Kwa Miguu Wa Jinsia Ya Kiume Ambaye Hakufahamika Jina Lake Na Kusababisha Kifo Chake Tukio Lililotokea Decemba 20 Mwaka Huu.
Amesema Kuwa Matukio Yote Mawili Yametokea Decemba 20 Ambapo Jeshi La Polisi Linaendelea Na Uchunguzi Dhidi Ya Matukio Hayo Na Kwamba Dereva Wa Gari Hilo Aina Ya Toyota Noa Ameshikiliwa Na Bado Yupo Mahabusu Katika Kituo Cha Polisi Makambako.
Katika Hatua Nyingine Kamanda Ngonyani Amezungumzia Hali Ya Ulinzi Na Usalaama Katika Kuelekea Skukuu Ya Christmas Na Mwaka Mpya Na Kwamba Ulinzi Umeimarishwa Kila Sehemu Ambapo Amewataka Wananchi Kuwa Makini Siku Ya Sikukuu Kwa Kuwalinda Watoto Wao Wasipotee.
Siku Chache Zimepita Wananchi Wa Vijiji Vya Igairo Na Ikondo Kata Ya Kichiwa Wakiwa Kwenye Eneo La Tukio Walikuwa Na Mtazamo Tofauti Kuhusiana Na Ajali Iliyosababisha Kifo Cha Askali Huyo Ambaye Alikuwa Na Gari Lenye Namba PT 0766 Ya Kituo Cha Polisi Makambako Ambapo Kamanda Ngonyani Amesema Uchunguzi Unaendelea Kubaini Kama Walikuwa Wangapi Kwenye Gari Hilo itakapobainika Hatua Zitachukuliwa Kwa Askali Hao.
Sanjari Na Hayo Katika Kuelekea Msimu Wa Sikukuu Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Limesema
Limejipanga Kufanya Doria Kila Maeneo Na Kuimarisha Ulinzi
Na Usalaama Wa Raia Na
Mali Zake Katika
Maeneo Yenye Mikusanyiko Ya Watu Ili
Kuzuia Kusijitokeze Athari,Vurugu
Na Kuchochea Fujo Na Uvunjifu Wa
Amani Msimu Wa Sikukuu Za Krismas Na
Mwaka Mpya.
Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe SACP Fulgence
Ngonyani Amesema Kuwa
Miongoni Mwa Maeneo Ambayo Jeshi Linatarajia Kuimarisha
Ulinzi Ni Pamoja Na Sehemu
Za Nyumba Za Ibada,Kufanya Misako Kwenye Nyumba Za Kulala
Wageni Ili Kudhibiti Na
Kubaini Watu Wanaohusika Na Vitendo Vya Unyang'anyi Wa
Kutumia Silaha Na Utekaji
Magari.
Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Jeshi La Polisi Pia Linaendelea Kutoa Elimu
Ya
Polisi Jamii Kwa Wananchi Hasa Katika Kipindi Hiki Cha
Sikukuu Kwamba Wanatakiwa Kuto acha Nyumba Zao Pasipo Uangalizi Pamoja Na Kutaka Vijana Kutojiingiza Kwenye
Vishawishi Vya
Makundi Ya Uharifu Na Tabia Ya
Kushinda Na Makundi Vijiweni Na
Uzururaji.
Katika Hatua Nyingine Jeshi La Polisi Limewataka Wamiliki Na
Madereva Wa Vyombo Vya
Moto Mkoani Hapa
Kuacha Kuendesha Vyombo Vya Moto Wakiwa Wamelewa Pombe Na
Hatua Kali Za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Ya Watakao
Patikana Wakiendesha Gari Wakiwa
Wamelewa Pombe.
Hata Hivyo Wananchi Wametakiwa Kutii Sheria Bila Shuruti Kwa
Kuwalinda Watoto Wao
Wakati Wakielekea Kwenye Sherehe Za Krismasi Na Mwaka Mpya
Ili Kuwalinda Watoto Wao
Wasipatwe Na Athari Za Barabarani Zinazoweza Kujitokeza
Katika Kipindi Hiki Cha Sikukuu.
No comments:
Post a Comment