Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na waziri mkuu Pinda ,Kushoto katika moja ya shughuli za serikali
, | |||
Rais Kikwete akimrekebisha kanzu waziri mkuu Pinda . ..................................................... NALAZIMIKA kutoa ushauri kwa mtoto wa mkulima waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya taarifa na mapendekozi yaliyosomwa bungeni na makamu mwenyekiti wa PAC Deo Filikunjombe na ile taarifa ya PAC iliyosomwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe hakika nakuwa wa kwanza kukushauri kurudi kijijini kusimamia shughuli zako za ufugaji nyuki. Hainiingii akilini hata kidogo kwa waziri wangu Pinda fedha hizo zikahamishwa na kugawana na watu bila wewe kuwajibika katika nafasi yangu labda utuambie watanzania kama wakati huo wewe ulikuwa likizo . Vinginevyo hata bila kusubiri wabunge kesho kuweza kuamua inafaa kujiwajibisha mwenyewe kwa kuachia ngazi ndani ya masaa 12 baada ya mapendekezo ya Filikunjmbe na kamati yake. Amina naungana na kamati ya PAC kuwa uteuzi wa mwanasheria mkuu utenguliwe afikishwe mahakamani huku waziri Mkuu alidai fedha za Escrow siyo za Serikali hivyo kumbadili waziri mkuu siyo jambo la ajabu hivyo Pinda akubali kuachia ngazi kama uwajibikaji Ila pia Bodi ya Tanesco ivunjwe Maswi imesababisha hasara kwa uzembe wake uteuzi wake usitishwe. anasema wachukuliwe hatua kupitia ibara ya 132,Naibu Waziri wa Nishati na Madini Masele achukuliwe hatua na waziri wa Nishati na Madini alikuwa dalali hivyo achukuliwe hatua mamlaka itengue nafasi yake Ila nasema kuchukuliwa hatua iwe ni pamoja na kufilisiwa mali zao zote na kutoruhusiwa tena kuongombea hata nafasi ya ujumbe kwa hawa na waziri wao Pinda . |
No comments:
Post a Comment