Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, November 26, 2014

Mgogoro wasababisha wanafunzi 400 kuacha masomo na 10 kupata mimba,mkoani Manyara



Wanafunzi 387 wa vijiji vya kata ya nambisi wilayani mbulu mkoani manyara wanaosoma katika shule ya sekondari ya kata ya Murray wamelazimika kuacha masomo baada ya  kushindwa kutembea umbali mrefu wa  zaidi ya km 30 wa kwenda na kurudi  kila siku kutokana na wanachi wa vijiji hivyo kuibua mgogoro  wa kutaka kila kijiji kujenga shule yake.
 
Makamu mkuu wa shule hiyo Bw.Denis Lohay amesema baada ya wananchi wa vijiji vya amoa,hhayloto na kwermusl kuigomea serikali akiwemo mkuu wa wilaya hiyo kuwataka kujenga shule ya sekondari ya kata mpya katika kijiji cha hhayloto baada ya kuanzishwa kwa kata mpya ya nambisi mvutano huo pia umechangia msongamano huku wasichana 10 wakipata mimba katika kipindi cha mwaka jana.  
Kufuatia kuwepo kwa mvutano huo uliosababisha kila kijiji kuanza ujenzi wake kwa madai kamati ya kata kutowashirikisha  wananchi  wa vijiji hivyo na kuibuka kwa mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu sasa kila kijiji kikiamua mipango yake baadhi ya wananchi wa vijiji cha amoa na kwermusl wamemueleza mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Zacharia Isaay  hawatabadili uamuzi huo kutokana na uwezo waliokuwa nao.  
Nae mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wilayani humo Bw.Zacharia Isay amesema serikali imetoa kibali cha ujenzi wa shule ya kata ya hhayloto sanjari na maabara,lakini pia akalazimika kuvunja mzizi wa fitna kuruhusu ujenzi wa shule katika kijiji cha amoa mara baada ya wananchi hao kugoma kuchangia na kudai watajenga shule yao bila ya msaada wa serikali.
 
edited by fredy mgunda

No comments:

Post a Comment