Afisa Ushirika Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Thomas Nyamba Ametolea Ufafanuzi Kuhusiana Na Kufufuliwa Kwa Chama Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe Ambacho Hapo Awali Kilikuwa Kikiitwa NJOLUMA Ambapo Kwa Sasa Kinaitwa Chama Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe.
Akizungumza Afisa Ushirika Huyo Bwana Nyamba Amesema Kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe Kitakuwa Kinahudumia Halmashauri Zote Sita Za Mkoa Wa Njombe Ambapo Kwa Kuanza Chama Hicho Kimeanza Kutafuta Fedha Kwaajili Ya Kuanza Zoezi La Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima.
Bwana Nyamba Amesema Kuwa Kila Halmashauri Inayolima Mahindi Imewekewa Kituo Cha Kukusanyia Mahindi Isipokuwa Wilaya Ya Makete Na Kwamba Kwa Wilaya Ya Njombe Kituo Cha Kukusanyia Mahindi Kipo Matembwe,Nyombo Na Ninga.
Amesema Kuwa Halmashauri Ya Wilaya Ya Ludewa Kituo Kitakuwepo Mlangali ,Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kituo Kitakuwa Luponde,Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Kituo Kipo Kwenye Chama Cha Msingi Cha Makambako Na Wanging'ombe Kipo Mambegu Ambavyo Vituo Hivyo Vitakusanya Mahindi Kwa Maeneo Yanayovizunguka Yote.
Bwana Nyamba Amesema Kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe Kimefanikiwa Kupata Mkopo Toka Benk Ya CRDB Wa Shilingi Milioni Mia Nne Ambao Unasaidia Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima Ambapo Mkopo Huo Hautosherezi Matakwa Ya Kununua Mahindi Kwa Wingi.
Aidha Bwana Nyamba Ametoa Wito Kwa Wakulima Kushikamana Ili Kukikuza Chama Hicho Ambapo Amesema Kubadilishwa Kwa Jina La Njoruma Kumetokana na Changamoto Ambazo Chama Hicho Kilizipata Hapo Awali Na Wajumbe Wakaamua Kubadili Jina Hilo Lisiwepo Kabisha Badala Yake Liwepo La Chama Kikuu Cha Ushirika.
No comments:
Post a Comment