· Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10.
· Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali” imeandaa
matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia
elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati
shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.
Matembezi
hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau
mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa
moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.
Akiongea
kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema
“wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na
kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa
njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari
ameshachangia.
Na
sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia,
marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha
watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri
“Lengo
ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na
kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”
Tutafanya
Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze
kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana
katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa
kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.
Tunatoa
wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi
haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi
ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora
,katika mazingira mazuri na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa
Airtel
chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi
katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa
wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king
Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi
imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili
ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu
ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.
No comments:
Post a Comment