Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, August 1, 2014

MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE YAMHUKUMU KIFUNGO CHA NJE MIEZI SITA JELA

Mahamakama ya Wilaya ya Njombe leo imemuhukumu kifungo cha nje miezi sita mkazi mmoja wa kijiji cha Makoga Anton Evarist Ngigwa ambaye alikuwa alishitakiwa  kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya  aina ya bangi gramu mbili.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali ambae jina lake hakutaka litajwe wazi kwa madai kuwa hajaruhusiwa na  Mwanasheria wake mkuu wakili huyo ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo mei 16 mwaka huu akiwa kijiji cha makoga.

Aidha Wakili huyo  amesema kuwa mtuhumiwa alipofikishwa katika mahakama hiyo tukufu alikili kutenda kosa na kwamba amekuwa akitumia madawa hayo aina ya bangi ili apate nguvu za kufanyia kazi  ya kupasua mbao.

Wakili huyo ambaye jinalake hakutaka lisikike kwenye vyombo vya habari ameiomba mahakama impatie adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia madawa kama hayo.

Kwa upande wake mshtakiwa bwana Anton Evarist Ngigwa ambaye amekuwa gerezani kwa muda wa miezi miwili akijitetea  ameiomba mahakama hiyo isimpe adhabu kali kwa kuwa anatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI,Pia anafamilia inayomtegemea wakiwemo wazazi wake ambao wapo Wilayani Mufindi.

Hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Njombe Josiah Samuel  amesema kwa  kuzingatia utetezi wa mshtakiwa huyo Mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo na atafungwa kifungo cha Nje miezi sita na hatakiwi kutenda kosa lingine kwa kipindi cha miezi sita.

Katika hatua nyingine mahakama hiyo imeahirisha kesi  ya kuvunja na kuiba mali mbalimbali za Jesca Mdeka mkazi wa Mtaa wa Ramadhani  hadi augost 11 inayomkabili bwana Ephroni Tweve ambaye alikamatwa na kikosi cha ulinzi shilikishi  akiwa na mali za dukani majira ya usiku anazodaiwa kuziiba maeneo ya mtaa wa Posta mjini Njombe.

Mwendesha mashtaka  wakili wa serikali ambaye jina lake hakutaka litajwe kwenye vyombo vya habari kwa kuwa hakuruhusiwa na mwanasheria mkuu ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo machi 22 majira ya usiku na kukamatwa na kikosi cha ulinzi shilikishi cha mtaa huo na kupelekwa katika kituo cha polisi ambako mlalamikaji alikwenda kuzitambua mali zake.

Kwa upande wake mshtakiwa  bwana Ephroni Tweve amekanusha kuhusika na kosa la kuvunja na kuiba mali hizo huku akiwalalamikia  waendesha mashtaka kwa kumfundisha mlalamikaji cha kwenda kuzungumza akiwa mahakamani na kumuelekeza mali za kuonesha kama kielelezo mbele ya mahakama ambapo Mwendesha mashtaka amesema mlalamikaji anahaki ya kukumbushwa mali alizoibiwa.

No comments:

Post a Comment