Friday, August 1, 2014
WANANCHI LUGENGE WATARAJIA KUONDOKANA NA TATIZO LA MAJI YA BOMBA
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA LUGENGE BWANA PAULINUS MGAYA AKIZUNGUMZA NA UPLANDS FM
Hatimaye wakazi wa vijiji vya Kata ya Lugenge Wilayani Njombe wanatarajia kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji ya bomba baada ya kufanyika kwa jitihada za kuchangia mradi wa maji ambao unatekelezwa katika kata hiyo.
Akizungumza na Uplands fm mwenyekiti wa Kijiji cha Lugenge bwana Paulinus Mgaya amesema mradi huo ulianza mwaka 2013 na kutarajia kukamilika augost mwaka huo Ambapo kutokana na wakandarasi kutolipwa malipo yao kwa wakati imepelekea kushindwa kukamilika kwa muda uliopangwa.
Aidha bwana Mgaya amesema mradi huo unatarajia kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili unaotekelezwa kwa ushirikiano wa wananchi na Serikali Ambapo wananchi wamechangia shilingi milioni hamsini ambazo zimehifadhiwa katika akaunti benki ya kijiji kwaajili ya matumizi ya ujenzi wa mradi huo.
Hata hivyo mwenyekiti huyo amesema pamoja na wananchi kuchangia fedha kwaajili ya Mradi huo pia wamechimba mitaru ya kutandika mabomba ya maji yenye umbali wa takribani kilomita 20 na tayari mkandarasi amekwishaanza zoezi la kuweka mabomba na matenki mawili ya maji yamekwisha kamilika.
Kwa Muda mrefu wakazi wa kata ya Lugenge wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa miundombinu ya maji ya bomba ambapo walilazimika kufuata huduma ya maji kwenye mito na visima ambayo si salaama, hivyo kukamilika kwa mradi huo utakaohudumia vijiji vinne utasaidia kutatua changamoto hiyo katika vijiji vya Kiyaula,Utaringolo,Lugenge na kisiro na tayari umefika kijiji Cha Lugenge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment