Monday, August 11, 2014
FAMILIA YA AKINA SOKOLO NA MUHEMA WAMEWASHUKURU WALE WOTE WALIOSHIRIKI MAZISHI YA MAMA YAO MPENDWA ATUPELYE SOKOLO ALIYEFARIKI JULY 10.2014 AKIWA KIBENA MJINI NJOMBE
MWILI WA MAREHEMU UNAPELEKWA KABURINI TAYARI KWA MAZISHI
KWAYA YA WAIMBAJI WA KUTOKA KANISA LA WASABATO NJOMBE
WACHUNGAJI WA KUTOKA KANISA LA SABATO NJOMBE WAKIOMBA KABLA MWILI WA MAREHEMU ATUPOKILYE SOKOLO HAUJAANZA KUZIKWA
HAWA WANANDUGU WAKITENGENEZA KABURI LA NDUGU YAO ATUPOKILYE SOKOLO
EDWARD SOKOLO AKISOMA HISTORIA YA MAREHEMU SHANGAZI YAKE BAADA YA MAZISHI KUFANYIKA
AFISA MTENDAJI WA MITAA YA KIBENA OTMARY MBANGALA AKIWA NA MWENYEKITI WA MTAA WA HOSPITALI PASCAL KADUMA WAKATUMIA NAFASI HIYO KUWATAKA WANANCHI KUCHANGIA MCHANGO WA CHAKULA SHULENI NA KUIMARISHA ULINZI SHILIKISHI KUTOKOMEZA UHARIFU.
WA UPANDE WA KULIA NI EDWARD SOKOLO,WA PILI KUTOKA KULIA NI ASHERY MHEMA NA WA TATU KUTOKA KULIA NI DAUD UHAHULA WOTE NI NDUGU
HAPA NI KIKAO CHA KIFAMILIA BAADA YA MAZISHI KUFANYIKA NA HAPA NI SIKU YA PILI
WA UPANDE WA KULIA NDIYE ALIYEFARIKI TAREHE 10 MWEZI WA SABA MWAKA 2014 ATUPOKILYE SOKOLO AMEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 96 NA WA PILI KUTOKA KULIA NI MDOGO WAKE AMBAE ALIFARIKI MIAKA TAKRIBANI MINNE ILIYOPITA ANAITWA JUDITH SOKOLO MAMA NA FAMILIA YA UHAHULA.
AFISA MTENDAJI WA MITAA HIYO AKATUMIA NAFASI HIYO KUWATAKA WANANCHI KUPELEKA CHAKULA SHULENI .
Afisa mtendaji wa mitaa ya kibena bwana Otmary Mbangala amewataka wananchi wa mitaa hiyo kuchangia chakula cha watoto wa shule za msingi Ujamaa na Kibena na kwamba kwa atakae kaidi kupeleka chakula hicho hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Akizungumza na wananchi wakati wa mazishi ya mama Atupokile Soholo afisa mtendaji wa mitaa ya Kibena bwana Mbangala amesema kuwa kutokana na baadhi ya wananchi kutoona umuhimu wa kuchangia chakula shuleni imepelekea serikali kuchukua hatua ya kuwasaka ambao hawajapeleka chakula hicho.
Bwana Mbangala amesema kuwa wakati shule zikitarajia kufunguliwa jumatatu ya wiki ijayo shule ya msingi Kibena na Ujamaa zimebakia na akiba kidogo ya chakula jambo ambalo limeulazimu uongozi wa mitaa hiyo kuchukua hatua ya kuwatafuta ambao hawakuchangia huku uchangiaji wa awamu ya pili ukianza kwa wananchi wote.
Katika hatua nyingine afisa mtendaji huyo amewataka wananchi kutolazi wageni kwenye nyumba zao pasipo taarifa kwa viongozi ambapo hali hiyo inafuatia kuwepo kwa matukio ya wizi wa mali uliokithili katika mitaa hiyo na kuwataka kutoa taarifa kwa viongozi mapema watakapo baini viashiria vya uharifu kutokea.
Mazishi ya Mama yake na Mwinjilisti wa kanisa la Advertist la Sabato Ashery Mhema Marehemu Atupokile Soholo yamefanyika july 10 ambapo alifariki july 9 akiwa na umri wa miaka 96 na kuelezwa kuwa marehemu huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo TB,Taiphoid, mkanda wa jeshi na hadi kufariki kwake alikutwa na ugonjwa wa maralia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment