RPC NJOMBE AKIWA WODINI BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA
HII NI BARABARA YA KUINGIA HOSPITALI YA KIBENA YA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIMPA POLE RPC KWA AJALI ILIYOWAKUTA
MAJERUHI WA AJARI HIYO DEREVA WA RPC NWAKA SEME AKIONGEA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA WODINI
DIWANI WA VITI MAALUM TARAFA YA NJOMBE MJINI BI.JENE NGENZI AKIWA NA MWENZAKE WAKIELEKEA KUMUONA RPC WODINI
HUYU NDIYE RPC MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI ANAENDELEA VIZURI NA DEREVA WAKE
GARI LA RPC LILILOPATA AJALI
ALIYEKUWA MLINZI WA RPC GEORGE STEPHANO MATIKO AMBAYE AMEFARIKI KWA AJALI
HILI NI GARI LA RPC AMBALO LIMEPATA AJARI BAADA YA DEREVA WA GARI LA RPC KUMKWEPA MWENYEGARI AINA YA KENTER ALIYEKUWA MBELE YAO NA HATIMAYE KUTOKEA KWA AJALI HIYO.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani Ameelezea Chanzo cha Ajali Iliyowapata Jana Usiku na Kusababisha Kifo cha Mlinzi Wake George Stephano Huku Dereva wa Gari Walilokuwa Wakisafiria Akijeruhiwa Sehemu za Kichwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Akiwa Amelazwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe SACP Ngonyani Amesema Ajali Imesababishwa na Gari Aina ya Kenta Ambalo Lilikuwa Mbele Yao Kuhama Njia na Kuwafata Upande Wao Jambo Ambalo Lilisababisha Gari Lao Kuacha Njia na Kupinduka, Kama Anavyoeleza.
Naye Dereva wa Kamanda wa Polisi Nwaka Seme Amesema Licha ya Kumwashia Taa Dereva wa Gari Aina ya Kenta Kumwashiria Kuwa Anakiuka Sheria Pamoja na Kujitihada za Kumkwepa Ndipo Alipohama Njia na Kugonga Nguzo ya Umeme , na Hapa Anaeleza.
Kwa Upande Wake Daktari wa Zamu wa Hospitali ya Mkoa Dkt. Dickson Haule Amekiri Kuwapokea Majeruhi Wawili Pamoja na Maiti Moja na Kusema Kuwa Hali za Majeruhi Zinaendelea Vizuri Kama Anavyoeleza
No comments:
Post a Comment