Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 1, 2014

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI NJOMBE LEO.

 








GASTON MSIGWA MWANDISHI WA TBC  AKIHOJI MASWALI YA UELEWA.

Serikali Imesema Licha ya Kukabiliwa na Changamoto Kubwa ya Fedha Kwa ajili ya Kufanya Maboresho Katika Daftari la Kudumu La Wapiga Kura Lakini Inaendelea Kukabiliana Nalo Katika Kufanikisha Suala Hilo Muhimu.

Kuli Hiyo Imekuja Wakati wa Semina ya Siku Moja Kwa Waandishi wa Habari Katika Mkoa wa Njombe Iliyofanyika Leo Mjini Njombe Juu ya Mpango wa Serikali wa Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Katika Maeneo Yote Hapa Nchini.

Akizungumza Wakati wa Ufunguzi wa Semina Hiyo ya Tume ya Uchaguzi Iliyolenga Katika Masuala ya Uboreshaji wa Daftari Hilo Kwa Waandishi Habari Jaji Mstaafu John Mkwawa Kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Amesema Kuwa Tume Hiyo Inaendelea Kukabiliana na Changamoto Hizo Ikiwemo Ugumu wa Mawasiliano Katika Mazingira Tata Wakati wa Uhamasishaji.

Aidha Jaji Mstaafu  Huyo Amesema Kuwa Serikali Inatambua Mchango Mkubwa wa Wanahabari Hapa Nchini Katika Kufikisha Ujumbe Sahihi Kwa Wananchi Wengi Zaidi Katika Masuala Mbalimbali Likiwemo la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Pamoja na Uchaguzi Katika Kusaidiana na Serikali Juu ya Suala la Chaguzi Mbalimbali.

Wakihoji Maswali Mbalimbali Katika Semina Hiyo Kwa Makamisheni wa Tume Hiyo Baadhi ya Wanahabari Mkoani Njombe Wamesema Kuwa Tume ya Uchaguzi Inawajibu wa Kuhakikisha Inaangalia Njia Mbadala ya Kuhakikisha Inaboresha Mawasiliano Katika Maeneo Ambayo Yamekuwa Yakikabiliwa na Changamoto Hiyo Hususani Katika Wilaya za Ludewa na Makete Ambako Ndiko Suala la Mawasiliano Limekuwa Kikwazo Katika Kukuza Uchumi wa Taifa na Mtu Mmoja Mmoja.

No comments:

Post a Comment