Friday, July 4, 2014
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO DKT PINDI HAZARA CHANA ATARAJIA KUTEMBELEA HOSPITALI YA KIBENA NA MAKAMBAKO
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii,Wanawake,Jinsia na Watoto Dkt Pindi Hazara Chana Kesho anatarajia kufanya ziara ya siku mbili wilayani Njombe ambapo pamoja na mambo Mengine atatembelea Shule ya Msingi Uwemba na kukabidhi Vitabu vya Masomo mbalimbali na kuzungumza na wanafunzi wakiwemo yatima.
Akizungumza na Uplands fm Naibu Waziri Chana Amesema Ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya masomo kwa Watoto wa shule wa shule za msingi ambapo Baada ya kutoka katika shule ya msingi Uwemba anatarajia kutembelea wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Kibena ili kubaini Changamoto zinazoikabili hospitali hiyo pamoja na wagonjwa wake.
Akiwa Wilaya ya Njombe Dkt Chana pia anatarajia kutembelea Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Wilayani Hapa pamoja na kutembelea Hospitali ya Makambako na kuzungumza na wagonjwa na wataalamu wa Hospitali hiyo ambako atakagua Sera ya Masuala ya Jinsia na Mtoto kama Inatekelezwa Ipasavyo kwa makundi yaliolengwa.
Aidha Pindi Chana Ameendelea kuwasihi wazazi na Walezi kutowanyanyasa watoto wote wakiwemo yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi huku Vijana wakitakiwa kuwaheshimu wazazi wao kwa kuwatimizia mahitaji muhimu wazee ambao hawana uwezo kwa kushirikiana na jamii inayozunguka maeneo waliopo wazee hao.
Naibu waziri Chana pia Amekemea vikali tabia ya baadhi ya jamii inayoendekeza imani za kishirikina na kwamba kitendo hicho kinachangia kwa kiasi kukubwa kukosesha amani wa watu Vikongwe ambapo serikali za mitaa na vijiji wametakiwa kuchukua hatua kali za kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watakapo baini baadhi ya watu wanatishia usalaama wa wazee vikongwe.
Ziara hiyo inatarajia kufanyika july 5 na 6 mwaka huu na kwamba Ziara hizo za Naibu Waziri Wa Maendeleo ya Jamii,Wanawake,Jinsia na Watoto Dkt Pindi Chana ni Muendelezo wa ziara zake za kila siku hapa Nchini ambazo hulenga kukagua maendeleo ya watoto,wanawake na makundi mbalimbali ya kijamii .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment