Friday, July 4, 2014
MAMLAKA YA MAJI NJOMBE MJINI NJUWASA YAWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA KUVUJA KWA MAJI NA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI NJOMBE MJINI DAUD MAJAN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji taka na safi mjini Njombe Daud Majani amewataka wananchi kutoa taarifa za uvujaji wa maji na uharibifu wa miundombinu ya maji ili kutafutiwa ufumbuzi haraka na kufikisha huduma stahiki kwa wateja wake.
Akizungumza na Uplands fm Mkurugenzi huyo bwana Majani amesema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wananchi wanaoingiza huduma hiyo pasipo mamlaka hiyo kutambua matumizi hayo na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo ili kuwachukulia hatua za kisheria pamoja na kukosekana kwa huduma za maji.
Aidha bwana Majani amesema kuwa Mradi wa maji wa kutoka chanzo cha Mto Nyenga tayari amaandalizi yalikwisha anza kwa kutengeneza miundombinu ya maji ambapo amewatoa hofu wananchi juu ya kukamilika kwa mradi huo na kwamba unatarajia kukamilika wakati wowote mwaka huu.
Amesema kuwa mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa vyanzo vya kutosha vya maji katika msimu wa kiangazi na kwamba imejipanga kikamilifu kuhakikisha inatatua kero za wananchi ambazo zimetoka zikiwakabili kwa muda mrefu.
Kwa upande wao wananchi mjini Njombe wameshukuru kwa hatua ambayo imefikia katika utekelezaji wa mradi wa maji Nyenga ambapo wameomba serikali kuharikisha utekelezaji wake ili kupunguza kero ya maji ambayo imekuwa ikiwakabili wananchi Mjini Njombe kwa muda mrefu msimu wa kiangazi.
Tatizo la kukosekana kwa miundombinu ya kutosha ya maji mjini Njombe ni la Muda mrefu ambapo hali hiyo inatokana na ongezeko kubwa la idadi ya wakazi ikiwa miundombinu ya maji inayotumika bado ni ile iliyoimairisha mwaka 2002 wakati idadi ya watu ikiwa ndogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment