Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, July 9, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO DKT PINDI HAZARA CHANA AENDELEA NA JITIHADA ZA KUTEMBELEA HOSPITALI NA WAGONJWA HAPA NCHINI









 NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE ,JINSIA NA WATOTO PINDI CHANA AKIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA NJOMBE YA KIBENA

 JITIHADA ZA SERIKALI ZA KUJENGA MAWODI MAKAMBAKO BADO ZINAENDELEA NA HATUA HIYO INAENDELEA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI MKOANI NJOMBE.





 NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE ,JINSIA NA WATOTO AKIWA KWENYE MAWODI YA WAGONJWA MAKAMBAKO



 PEPETUA NGONGI AKITOA NENO

 HAWA NI WAFANYAKAZI WA AFYA MAKAMBAKO





 HAPA NAIBU WAZIRI AKIWA HOSPITALI YA MAKAMBAKO

Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii,Wanawake,Jinsia na Watoto  Pindi Hazara Chana ameahidi kuzifikisha changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali ya mkoa wa Njombe ya Kibena na hospitali ya halmashauri ya Makambako ili serikali iweze kuharakisha uboreshaji wa miundombinu ya maeneo hayo.

Akizungumza na Wagonjwa mbalimbali akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Njombe Naibu Waziri Chana amepokea malalamiko ya akina mama wajawazito wa hospitali ya Kibena kuhusiana na kukosekana kwa vyumba na vitanda vya kujifungulia na kwamba kitanda kimoja wanalazimika kulazwa watu wawili.

Aidha Naibu waziri Chana amewaomba wagonjwa waliopo katika vituo na hospitali mbalimbali mkoani Njombe kuvumilia wakati serikali ikiendelea kuzitatua baadhi ya changamoto zilizopo chini ya uwezo wao  huku akiwataka wakuu  wa Idara kufuatilia baadhi ya watumishi wa serikali hususani sekta ya afya ambao wamekuwa wakikaa nje na vituo vyao vya kazi kwa nyakati za zamu za usiku.

Akizungumza mara baada ya Naibu Waziri huyo kukamilisha zoezi la kuwatembelea wagonjwa wa Hospitali ya Kibena  Dr Godfrey Baradona ameshukuru  kwa kutembelewa  na Naibu Waziri huyo na kuomba kutatuliwa baadhi ya changamoto zinazowakabili wagonjwa ikiwemo chumba cha kuhifadhia maiti na kuongezewa wodi la akina mama ili kuepukana na akina mama kulala watu wawili kitanda kimoja.

Kwa upande wao akina mama wajawazito  wamepongeza kwa hatua ambayo imeanza kufanywa na serikali ya kuboresha huduma za matibabu kwa wajawazito kupatiwa  huduma ya matibabu bure na mtoto ambapo changamoto kubwa inayowakabili ni kulala kitanda kimoja watu wa wili  huku wajumbe walioongozana na Naibu waziri huyo wakiomba viongozi wa serikali kufanya ziara za ghafra kutembelea vituo na hospitali mbalimbali mkoani Njombe  nyakati za usiku kikiwemo kituo cha Afya cha Njombe mjini kubaini watumishi wa zamu za usiku kama wanakuwepo masaa yote.


No comments:

Post a Comment