DIWANI WA KATA YA LUPEMBE BI.TWILUMBA WAPALILA ENZI ZA UHAI WAKE NA HAPA ALIPOKUWA AKIJIBU MASWALI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE ALIPOKUWA AMETEMBELEA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Lupembe Wilayani Njombe Bi .Twilumba Wapalila, Amefariki Usiku wa Kuamkia Leo Jijini Dar Es Salaam Alikokuwa Akipata Matibabu Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akitoa Taarifa za Msiba Huo Wakatia Akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Hii Leo , Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Valence Kabelege Amesema Marehemu Alikuwa Anasumbuliwa na Vidonda Vya Tumbo
Kufuatia Kifo cha Diwani Huyo Madiwani wa Halmashauri Hiyo Wamelazimika Kufupisha Kikao cha Baraza Hilo, Huku Mazishi ya Bi. Wapalila Yakitarajia Kufanyika Julai 11 Mwaka Huu.
Msiba Huu ni wa Pili Kwa Wananchi na Wanachama wa CCM Tarafa ya Lupembe Huku Ukiwa ni wa Tatu Kwa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Wilaya Baada ya Kifo cha Aliyekuwa Diwani wa Mfriga Kamilo Hongoli na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Adam Msigwa Pamoja na aliyekuwa katubu wa ccm Wilaya ya Njombe ambae alifia mkoani Mbeya akiwa likizo hapo mwaka jana.
Nako Mkoani Mbeya Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Redio na Luninga cha Sweet Emmanuel Joseph Mbuza Amefariki Usiku wa Kuamkia Leo Jijini Dar Es Salaam Huku Mipango ya Mazishi Inafanyika Nyumbani Kwa Kaka Yake Tabata Jijini Dar Es Salaam.
Wakati wa Uhai Wake Marehemu Emmanuel Joseph Mbuza Aliwahi Kuwa Mfanayakazi Katika Kituo cha Redio cha Mbeya Fm , Generation na LLB & MBA Chuo Kikuu cha Tumaini.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.
No comments:
Post a Comment