Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, July 10, 2014

BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA NJOMBE LA WATAKA WATENDAJI KATA NA VIJIJI KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO YA HALMASHAURI



 WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAKIWA KWENYE BARAZA HILO

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENCE KABELEGE AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA MKUTANO HUO




 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKITOA SALAAM ZA SERIKALI
 MAKAM MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE SHAIBU MASASI AMBAE NI DIWANI WA KATA YA MATEMBWE

 DIWANI WA KATA YA KIDEGEMBYE JULIUS SARINGWA AKIWASILISHA TAARIFA YA MAENDELEO YA KATA YAKE

 DIWANI WA KATA YA IKUNA VALENTINO HONGORI AKIWASILISHA TAARIFA YA MAPATO YA KATA YAKE



 KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE NAE AKIWASILISHA SALAAM ZA SERIKALI




Na Michael Ngilangwa
Baraza la madiwani la Wilaya ya Njombe limewaagiza watendaji wa kata kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kuhakikisha wanashiki kikamilifu katika ukusanyaji wa mapato katika maeneo mbalimbali ya magurio huku kata ambazo zimeshindwa kutimiza malengo ya halmashauri hiyo kuiga mfano wa kata nyingine zinazofanya vizuri.

 Kauli hiyo imetolewa kufuatia kuwepo kwa baadhi ya kata kusuasua kukusanya mapato kwenye mageti na magurio ya minada kutokana na watendaji wa kata kushindwa kuhudhuria kwenye magurio hayo na kuwaachia watendaji wa vijiji jambo ambalo limesababisha mapato ya kwenye magurio kutopatikana kwa wingi.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe  Valence Kabelege  amewataka watendaji kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kufungua masanduku ya maoni na kuyafungua mara kwa mara pamoja na kuhamasisha wananchi kutuma maoni yao juu ya malalamiko mbalimbali yanayowakabili.

Aidha mwekiti huyo Kabelege amewataka wakuu wa idara ya Elimu kutambua uwepo wa shule za awali kwa kupeleka walimu waliosomea kwani hadi sasa hakuna mchango wowote wa serikali kuhusiana na kupeleka walimu wa madarasa ya awali jambo ambalo limesababisha kutoanzishwa kwa shule hizo katika maeneo mbalimbali mkoani Njombe.

Akitoa salaamu za serikali kwenye mkutano huo wa baraza la madiwani mkuu wa Wilaya ya Njombe  b.Sarah Dumba amepongeza kwa jitihada zinazofanywa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao na kufanikisha kupata ushindi  wa  usafi Kitaifa ambapo amesema serikali imesisitiza wanafunzi wote kupata madawati katika sekta ya elimu na kuweka mazingira yake kuwa mazuri  na kukusanya mapato ya kutosha ili kutekeleza sera ya BRN.

Bi. Dumba amesema  serikali imeagiza kila shule ya sekondari  kuwa na maabara tatu   na ujenzi wa vyumba vya madarasa  vitakavyokidhi mahitaji ya wanafunzi  pamoja na viongozi hao kuhakikisha makusanyo  ya ndani yanapatikana kwa wingi ili halmashauri hiyo iweze kujiendesha na kwamba kila diwani anawajibu wa kusimamia mapato katika kata yake.

Kwa upande wao wajumbe wa baraza la madiwani wilaya ya Njombe wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi na ukusanyaji wa mapato wamesema wamefanikiwa kukusanya pesa toka kwenye vyanzo mbalimbali vikiwemo vya mageti  na ushuru wa vibanda mbalimbali vya biashara.

No comments:

Post a Comment