WATUMISHI WA HALMASHAURI ZA MJI NA WILAYA WAKICHANGIA HOJA
WATUMISHI WA HALMASHAURI ZA MJI NA WILAYA YA NJOMBE WAKIWA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AMBAE NI AFISA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI VENANCE MSUNGU AKISIKILIZA KWA UMAKINI MAELEZO YA WATAALAMU HAO.
AFISA LISHE WA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TAIFA CELESTINE MGOBA
AFISA LISHE TOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII TAIFA BI. GRACE MOSHI
Taasisi ya Chakula na Lishe Imezindua Mradi wa Kuongeza Virutubishi vya Madini Joto Kwenye Vyakula Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Ili Kukabiliana na Matatizo ya Udumavu Wakati wa Ukuaji wa Mtoto na Afya Kwa Ujumla.
Katika Uzinduzi Huo Uliowajumuisha Watendaji wa Idara Mbalimbali Katika Halimashauri ya Mji wa Njombe Ambapo Watendaj Hao Wametakiwa Kuufanya Mradi Huo Kuwa Endelevu Utakaosaidia Kupunguza Matatizo ya Utapiamlo Pamoja na Kufanya Jamii Kuwa Zenye Afya Bora.
Akizungumza Katika Ufunguzi Huo Afisa Lishe Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi,Grace Moshi Amesema Lengo la Mradi Huo ni Kuishinikiza Jamii Kutumia Vyakula Vilivyoongezwa Virutubisho Katika Familia Zao Ili Kuweza Kukabiliana na Magonjwa Yasiyouwa ya Lazima Kama Mtindio wa Ubongo Pamoja na Magonjwa Mengine.
Kwa Upande Wake Mtaalamu wa Lishe Kutoka Katika Taasisi Isiyo Kuwa Yakiserikali ya Food Print Bw,Joseph Nsoza Amesema Wamekwisha Kutoa Elimu Namna Virutubisho Hivyo Ambavyo Vitakuwa Vkitolewa Kwenye Maeneo ya Mashineni Pindi Mteja Anapoenda Kusaga Mahindi Ambapo Msagishaji Atapewa Virutubishi Hivyo Ili Kuchanganya Kwenye Mahindi ya Mteja Kulingana na Vipimo Vilivyopo Kabla ya Kusaga Mahindi Hayo
Bw,Nsoza Amesema Wamekwisha Kutoa Elimu Kwa Wamiliki Wate wa Mashine za Kusagisha Mahindi Namna ya Kutoa Vurutubisho Hivyo Katika Maeneo Yote ya Vijijini Ambapo Mteja Atachangia Kiasi Cha Shilingi 200 Pekee.
Katika Taarifa ya Hali ya Afya Iliyo Tolewa na Afisa Afya Kutoka Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bi,Bertha Nyigu Imebainiasha Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukuaji wa Kasi wa Tatizo la Utapiamlo Kwa Watoto Waliochini ya Umri wa Mwaka Mmoja Katika Mji wa Njombe Pamoja na Meneo Mengine.
Aidha Taarifa Hiyo Imesema Kuwa Katika Kipindi Cha Kuanzia Mwezi January Hadi May Mwaka Huu Jumla ya Watoto 20 Walilwazwa Kutokana na na Ugonjwa Huo wa Utapiamlo na Kati ya Hao Watoto 6 Wamepoteza Maisha Kutokana na Athari za Utapiamlo Kwa Watoto Waliochini ya Umri wa Mwaka Mmoja.
Kwa Upande Wake Kaimu Mkurugenzi Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw,Venance Msungu Ameipongeza na Kuishukuru Taasisi ya Chakula na Lishe Kwa Kuzindua Mradi Huo Katika Mji wa Njombe Ambapo Amesema Kuwa Atahakikisha Mradi Huo Ataufanya Kuwa Endelevu Kwa Kushirikiana na Wataalamu Mbalimbali Ili Kulet Tija Katika Jamii.
Mradi Huo Unatekelezwa Katika Mikoa ya Iringa,Njombe,Arusha Ambapo ni Katika Maeneo ya Halmashauri ya Mji Njombe,Iringa Vijijini,Kilolo,Karatu,na Monduli
No comments:
Post a Comment