Thursday, June 12, 2014
MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA TANESCO WILAYA YA NJOMBE AJIKUTA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU BAADA YA KUKABWA NA KAMBA ALIZOJIFUNGA WAKATI AKIFANYA MAREKEBISHO YA UMEME MTAA WA JOSHONI .CHANZO NI KUTEREZA KWA VIATU ALIVYOKUWA AMEVAA NA KUNING'INIA JUU MPAKA KUOKOLEWA NA WASAMALIA WEMA.
HII NI NGUZO AMBAYO ALIPANDA MTUMISHI HUYO
AFISA MTENDAJI WA MTAA WA JOSHONI AKIZUNGUMZA NA MASHUHUDA WA AJALI HIYO
HII NI MITA NA WAYA WA UMEME AMBAO ALIKUWA ANATAKA KUUNGANISHA
Mfanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Wilayani Njombe Ambaye Jina Lake Halikufahamika Mara Moja Amenusurika Kifo Baada ya Kutokea Hitilafu ya Umeme Wakati Akiingiza Huduma ya Umeme Kwa Mmoja wa Mteja Wao .
Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa Tukio Hilo Wamesema Ajali Hiyo Imetokea Juni 10 Mwaka Huu Majira ya Saa 11 Jioni Mtaa wa Joshoni Mjini Njombe na Kueleza Kuwa
Mfanyakazi Huyo Alikutwa na Mkasa Huo Baada ya Viatu Alivyokuwa Amevaa Kuteleza.
Wakiongea Mara Baada ya Kutoa Msaada Baadhi ya Wananchi na Wafanyakazi wa TANESCO Wamesema Ajali Hiyo ni ya Kawaida , Huku Afisa Mtendaji wa Mitaa ya Joshoni na Mpechi Bi. Isabela Malangalila Akisema Kuwa Alipata Taarifa za Ajali Hiyo Lakini Alipofika Eneo la Tukio Tayari Mfanyakazi Huyo Alikuwa Ameokolewa.
Andrew Lukoto ni Mhasibu wa shirika hilo wilaya ya Njombe ambae alikaimishwa baada ya makaimu meneja wote wawili kuwa safarini amesema kuwa yeye tangu alipoachia ofisi hiyo hakuweza kupatiwa kuwepo kwa taarifa za tukio hilo.
Uplands Redio Imefanya Jitihada za Kuwatafuta Viongozi wa TANESCO Kuzungumzia Suala Hilo Bila Majibu Sahihi, Huku Kaimu Meneja Andrew Lukoto Akieleza Kuwa Tangu Akabidhiwe Ofisi Leo Asubuhi Hafahamu Kama Kuna Mfanyakazi Alipata Ajali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment