MKUU WA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA MWALI FRANCE MNG'ONG'O AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA WATU TAPELI HAO
VIBAKA WAKIWA KATIKA OFISI YA MTENDAJI IDUNDILANGA BAADA YA KUKAMATWA NA WANANCHI WA MTAA HUO
VIJANA HAWA WAMEDAI KUTUMWA NA KAKA YAO AMBAE ANAFANYA KAZI HIYO YA KUOMBA MISAADA ILI KUPATA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU
WA KWANZA KUTOKA UPANDE WA KULIA NI FRANK SHABAN MKAZI WA ITEWA MBEYA,WA PILI KUTOKA KULIA NI REONARD KATAMBA MKAZI WA TUKUYU MBEYA MTAA WA TANESCO NA WA TATU SHUKRAN ANGOLILE MKAZI WA TUKUYU MBEYA MTAA WA MABONDE
WA KWANZA KUTOKA UPANDE WA KULIA FRANK SHABAN HUYU ALIKUWA NA SIMU YENYE NAMBA ZA SIMU ZILIZOWEKWA KWENYE FOMU HIYO ILIYOGONGWA MHURI WA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA AMBAO NI WA BANDIA
NAMBA HIZO KWENYE FOMU UKIPIGA ANAPOKEA KIJANA HUYO AMBAE ALIDAI YUKO MBEYA KUMBE ALIKUWA KATIKA SALOON ILIYOPO KARIBU NA KANISA LA ROMAN KATHOLIKI SALOON ZILIZOPO CHIPOLOPOLO
HII NI FOMU AMBAYO VIJANA HAO WALIKUWA WAKIITUMIA KUCHANGISHA MICHANGO HIYO NA WATU KIBAO WAMEKWISHA KUCHANGIA
Viongozi wa mitaa ya Idundilanga,Mpechi na Joshoni wamepiga marufuku kwa baadhi ya mabarozi kuchangisha michango ya misiba ambayo imetokea mikoa ya mbali na kuwataka wananchi kuwa makini na watu tapeli ambao wamekuwa wakitumia njia hiyo kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.
Hatua hiyo ya viongozi wa mitaa kuzuia michango isiyo pitishwa na viongozi wa mitaa wakiwemo watendaji na wenyeviti imekuja kufuatia kuwepo kwa baadhi ya wananchi kutumia sababu ya kufiwa kuwadanganya mabarozi wachangishe michango ya msiba kwa lengo la kujipatia kipato kwa njia ya Udanganyifu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watendaji wa mitaa ya Idundilanga,Mpechi na Joshoni Mashaka Lurambo na Isabela Malangalila wamesema michango ya msiba inayotakiwa kuchangiwa ni ile inayotokea katika eneo husika ama kupelekwa eneo hilo ambapo wamesema kuwa udanganyifu huo umekuwa ukifanywa na baadhi wa watu wanaodai wamefiwa na kuomba kuchangiwa huku wakidai Wamefiwa mbali na mazishi yanafanyika hukohuko jambo linalosababisha kushindwa kupata ukweli wake.
Akizungumzia suala la utapeli ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu afisa mtendaji wa mtaa wa Idundilanga Mashaka Lulambo amesema kuwa baadhi ya wananchi wa mtaa wa Idundilanga wamefanikiwa kuwakamata vijana watatu wakazi wa mkoa wa Mbeya ambao walikuwa wakichangishwa pesa kwa wananchi mjini Njombe wakidai wameshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mtu wa kuwasomesha huku wakitumia mhuri wa bandia wa shule ya sekondari Iyunga ili kujipatia pesa kwa njia hiyo.
Bwana Lulambo amewataja vijana hao ambao wanatokea Jijini Mbeya kuwa ni pamoja na Frank Shabani mkazi Itewe ,Reonald Katemba mkazi wa Tukuyu,Shukrani Angolile mkazi wa Tukuyu mtaa wa Mabonde mkoani Mbeya ambao walikamatwa wakati wakiomba msaada wa kuchangiwa mchango wa fedha kwaajili ya kuendelea na masomo wakiwa na Fomu iliyogongwa mhuri wa bandia wa mkuu wa shule ya sekondari Iyunga..
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya Sekondari Iyunga mkoani Mbeya Mwalimu France Mng'ong'o amesema kuwa anashangazwa kuona vijana hao wametumia jina la shule yake kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu na kwamba vijana hao hawatambui na wala hawajawahi soma shule hiyo na kuwataka wananchi kujiridhisha kabla ya kutoa mchango wao wa msaada pamoja na kuendelea kuonesha ushirikiano.
Zoezi la wananchi kuchangishwa michango ya misiba kwa baadhi ya mitaa mjini Njombe limekuwa likiendelea huku wananchi wakishindwa kufahamu mchango huo kama unakwenda kwenye msiba kutokana na baadhi ya mabarozi kuwachangisha shilingi elfu mbili kwaajili ya msiba ambao umetokea mbali na eneo husika na mazishi hufanyika nje na eneo hilo jambo ambalo linasababisha wananchi wa mitaa na kata husika kushindwa kuhudhuria na kutambua kama kweli kuna msiba ama sivyo kwa kuwa anaechangiwa kudai anakwenda kuzika mbali ili hali wenyeji hawamtambui marehemu anakoishi wala anakokwenda kuzikwa.
Mchango unaotakiwa kuchangiwa ni ule ambao msiba umetoka mbali na kuja kwenye eneo la mtaa ama kijiji husika wananchi wanapaswa kuchangia kwa kuwa watakuwa wanashuhudia kwa kuhudhuria mazishi na msiba unaotoka kwenye mtaa ama kijiji husika na kwenda kuzikwa sehemu nyingine iwe mkoa,wilaya za nje na kule marehemu alikokuwa akiishi wananchi wanapaswa kuchangia.walisema watendaji hao wa mitaa ili kuhepusha utapeli.
No comments:
Post a Comment