Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, June 3, 2014

TAMASHA LA UMOJA KWANZA LA FAANA LUDEWA




MA DJ  WAKIENDELEA NA KAZI YAO YA KUSETI MITAMBO YA MUZIKI WILAYANI LUEDEWA ALIYESHIKA MASHINE YAANI MIXER NI DJ PHIL KUTOKA UPLANDS FM RADIO AKIWAELEKEZA MA DJ WADOGO JUU YA KUITUMIA MIXER WAKATI WA KUPIGA MUZIKI AKIWA NA EMMANUEL MWAKA POTELA AMBAE NI MC KWENYE TAMASHA HILO WA UPANDE WA KUSHOTO ALIYEVAA TSHERT ILIYOANDIKWA NSALAAMA.

 WANANCHI WILAYA YA LUDEWA WAKIWA KATIKA KUSHUHUDIA WASANII MBALIMBALI WAKITUMBUIZA KWENYE TAMASHA LA UMOJA KWANZA WILAYANI HUMO









 HUYU NI MC WA TAMASHA LA UMOJA KWANZA  MAMA NYEUPE JINA LAKE HALISI PILI NYENJE
BURUDANI KALI TOKA KWA WASANII WA KUNDI LA KIBENA ARTS GROUP WAKIBURUDISHA UMATI WA WANANCHI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO WILAYANI LUDEWA AMBALO LILIBEBA UJUMBE WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI NI ZERO

Uplands fm radio kutoka Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na taasisi nyingene za binafsi na uongozi wa serikali  mkoa wa Njombe  imeandaa tamasha kubwa ambalo limelenga kuelimisha jamii mkoani humo juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kutembelea Wilaya zote za mkoa huo ambapo Jumamosi ya wiki iliyopita tamasha kubwa lilifanyika wilaya ya Ludewa.

Meneja wa kituo cha Radio Uplands fm Novatus Lyaluu amesema kuwa Tamasha hilo limeshilikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau  wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Mkoa wa Njombe watu wa Kuhamasisha matumizi ya Kondom  PSI Na kwamba tamasha hilo linatarajia kuendelea tena jumamosi ya wiki hii wilayani Makete na baadae Wanging'ombe na Makambako kwa kila Juma mosi.

No comments:

Post a Comment