Mwili wa Kijana huyo Ukiwa umefunikwa na Majani Kabla ya Kuchomwa Moto
Mwili wa Kijana huyo ukiwa unachomwa Moto na wananchi wa Eneo hilo
Akielezea Tukio Lilivyo tokea
Ng'ombe Walioibiwa
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
**********************
WAKATI vyombo mbali mbali
zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia
sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya.
Hali hiyo imezidi kujitokeza
baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na
kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja
wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio
hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo
chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya
Ilomba.
Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa
jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa taarifa kwa majirani ambao asubuhi
walijihimu kutafuta ambapo walipofika maeneo ya
Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na
mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
Alisema baada ya kusikia hivyo
waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na ndipo walipofika eneo la
Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na hao Ng’ombe.
Alisema Wananchi mbali mbali
walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana na eneo hilo kukithiri kwa
wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari
jambo lililowatia hasira na kuamua kumchoma moto.
Shuhuda huyo aliendelea kusema
baada ya kuanza kumchoma lakini katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho hadi alipookolewa na Askari
wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna
taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.
Endelea Kufuatilia hapa hapa.
KWA HISANI YA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment